Tuesday, August 25, 2015

WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM AZINDUA BODI YA PPF NA MAFAO MAPYA YA MFUKO

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja, mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sara Haule ikiwa ni malipo ya fao la uzazi wakatinwa uzinduzi wa bodi mpya ya PPF, sambamba na uzinduzi wa fao hilo la uzazi, Jumanne Agosti 25, 2015.
 Waziri Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho nwakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mfuko, sambamba na uzinduzi wa Fao la Uzazi, ambapo wanachama wawili wa Mfuko, Sara Haule na Caroline Kiswaga, walilipwa shilingi milioni 1 kila mmoja kama malipo ya fao hilo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, akitoa hotuba yake
 Waziri Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF

 Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za PPF, na Mamenejawaliohudhuria hafla hiyo, 
 Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku, akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake
 Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF
 Waziri Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Caroline Kiswaga, baada ya kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, (kushoto), akimkabidi kadi mpya ya uanachama wa Mfuko nhuo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya SDalum, wakati wa uzinduzi wa bodi na fao la uzazi, hafla iliyofanyika makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2015.
 Waziri Saada Mkuya, (kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, 
 Waziri Mkuya akiteta jambo na Erio wakati wa hafla hiyo
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,  Elihuruma Ngowi, (kulia), akifurahia jambo wakati waziri wa fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimtania Mwanachama wa PPF, Sara Haule, baada ya kupatiwa malipo ya shilingi milioni moja kama fao la uzazi

No comments: