Na IZACK MAGESA-Dar es Salaam
Taasisi ya isiryo ya
kiserikali TASWEP leo imetoa wito kwa jamii nzima kutokujihusisha na vitendo
vyovyote vinavyohusiana na maswala ya ukatili wa kijinsia wala unyanyasaji wa
aina yoyote katika jamii inatyowanguka.
Wito huo umetolewa leo
jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu NAFUTA RING’ONDI
wakati wa uzinduzi wa chuo kipya cha ustawi wa jamii Jijini Dar es salaam
ambapo amesema kuwa kuna Haja sasa ya jamii kuepoukana na mfumo Dume kwani ndio
chanzo cha vitendo chanzo cha vitendo hivyo vya ukatili katika jamii ambapo
ameongeza kuwa chuo hicho kimekuja ili kupambana na na hali hiyo ikiwa ni
pamoja na kuongeza elimu ya ustawi wa jamii katika nchi ya Tanzania.
Meneja wa Taasisi hiyo Bi STELLA MNGODO pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu NAFUTA RING’ONDI wakishirika katika kukata utepe kuashiria kwa uzinduzi wa chuo hicho kipya cha maswala ya ustawi wa Jamii nchini Tanzania |
Aidha akizungumza
katika uzinduzi huo meneja wa taasisi hiyo Bi STELLA MNGODO amesema kuwa kwa
sasa hapa nchini matatizo ya ukatili wa kijinsia ni mengi ambayo hasa huwakumba
zaidi watoto na kina mama hivyo wameamua kufungua chuo hicho ili kupunguza hali
hiyo ambapo amesema kuwa chuo hicho mpaka sasa kina wanafunzi 20 wanaosomeshwa
bure ambapo kinadhaminiwa na msaada wa watu wa marekani.
Aidha meneja huyo amewataka wanahabari nchini
kusaidia jamii katika kuandika na kureport matukio mbalimbali yanayohusiana na
jinsia nchini ili kusaidia zaidi katika kupambana na vitendo hivyo
No comments:
Post a Comment