Saturday, September 26, 2015

LHRC WAADHIMISHA MIAKA 20 YA UWEPO WAKE TANZANIA-PICHA ZIPO HAPA

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ambaye ni Jaji mstaafu wa mahakama ya Rufani Tanzania Jaji EUSEBIA MUNUO (kulia) Pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA wakizindua kitabu kipya cha Miaka 20 ya kituo hicho Jijini Dar es salaam kitabu ambacho kinaelezea mafanikio na historia nzima ya kutuo hicho tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC,profesa GEOFREY MMARI akizngumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa kituo hicho waliohudhuria katika hafla ya kusherehekea kutimiza miaka 20 ya kituo hicho Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho DK HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza amesema kuwa moja ya mafanikio ya miaka 20 ya kituo hicho ni kufanikiwa kuwafanya watanzania wengi kuanza kutambua na kujua jinsi ya kudai haki zao tofauti na zamani ambapo amesema kuwa kwa sasa kuna muamko mkubwa wa watu mbalimbali kuamua kudai haki zao pale wanapogundua wananyimwa jambo ambalo amelitaja kama mafanikio makubwa ya kituo hicho ndani ya miaka 20 pamoja na kuendelea kuwepo kwa vitendo vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.
Prof CHRIS PETER amabaye ni mmoja kati ya walioshiriki kuandika kitabu cha miaka 20 ya LHRC akielezea mambo yanayopatikana katika kitabu hicho
Onesmo Ulengurumwa mwanasheria kutoka katika kituo hicho Aikifafanua jambo kuhusu miaka 20 ya LHRC katika maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es salaam

Meza kuu





Picha nne za juu ni watoa burudani wa kwaya maarufu ya MWALUSANYA wakitoa burudani katiika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania nLHRC maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es salaam 




Wafanyakazi pamoja na wadau mblaimbali wa LHRC wakiwa katika hafla hiyo



Mgeni rasmi wa hafla hiyo ambaye ni Jaji mstaafu wa mahakama ya Rufani Tanzania Jaji EUSEBIA MUNUO akizngumzaa katika shughuli hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amekitaka kituo hicho kuendelea kuwekeza katika kuwasaidia Watanzania kataika maswala ya haki kwani bado kuna changamoto kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini hku akiwapongeza kwa kazi kubwa na inayoonekana iliyofanywa ndani ya miaka 20 ya kituo hicho


TUNASOMA-Wadau mbalimbali wakisoma kitabu cha miaka 20 ya LHRC ambacho kilizinduliwa katika hafla hiyo

Keki maalum ya maadhimishi ya miaka 20 ya LHRC








Vikundi vya ngoma vikitoa burudani

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa LHRC 

No comments: