Wednesday, September 2, 2015

MAGEUZI YA MIFUMO KANDAZIMIZI HAYAEPUKIKI-WANAHARAKATI WA TGNP

MWANAFEMINISTI KUTOKA NCHINI NIGERIA. PROF. AMINA MAMA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WANANCHI WALIOHUDHURIA TAMASHA LA JINSIA KWA MWAKA 2015 KATIKA VIWANJA VYA TGNP VILIVYOPO KATA YA MABIBO WILAYA YA KINONDONI JIJINI DARESALAAM,, PROF. AMINA MAMA ALISEMA KUTOKANA NA UCHAMBUZI  WA KIFEMINISTI AMBAO UMEFANYWA KUHUSU SERA ZA SOKO HURIA UMEONYESHA KUWA HAKUNA UHURU WOWOTE UNAOLETWA NA TAASISI ZA KIFEDHA.

WANAHARAKATI WA KIJINSIA WAKIFUATILIA HUTUBA YA PROF. AMINA MAMA KATIKA VIWANJA HIVYO VYA TGNP MAPEMA HII LEO, PROF. AMINA AMEWATAKA WANAWAKE HAO KUTOKATA TAMAA KWANI MABADILIKO HAYAJI WENYWE. KASI YA MABADILIKO INAHITAJI KUJITOA.
MKURUGENZI MTENDAJI WA MTANDAO WA KIJINSIA TGNP AKIFAFANUA BAADHI YA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI. AMESEMA MTANDAO WAKE HAUKO NYUMA KUHAKIKISHA KUWA INAFUATILIA KWA KARIBU NA KUTOA MAFUNZO KWA WABUNGE WANAWAKE ILI KUWAJENGEA UWEZO WA KUWASILISHA MASLAHI YA WANAWAKE KULE BUNGENI
SEHEMU YA WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO WAKIFUATILIA KWA MAKINI MADA KUTOKA KWA PROFESA HUYO, KATIKA HATUA NYINGINE PROF AMEWATANGA VIONGOZI WA KISIASA HUSUSANI WANAWAKE  WAWE MSTARI WA MBELE KUTETEA MASLAHI YA WANAWAKE.


PROF. AMINA MAMA AKIFAFANUA JAMBO KWA WANAHABARI, ALISEMA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MWANAMKE NI ENDELEVU NA ZINAHITAJI KUKUMBUSHA KILA MARA KWANI KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA KUTETEA MASLAHI YA WANAWAKE.

No comments: