TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana na vyombo vya habari mbalimbali kutaka kauli yetu
kuhusu mkutano wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Willbroad Slaa na
waandishi wa habari uliofanyika jana Hoteli ya Serena na kutangazwa moja kwa
moja na vituo vya televisheni na radio, tunapenda kusema ifuatavyo;
Tumemsikia Dkt. Slaa. Kwa sasa nguvu, akili, mioyo na miili ya
wapiganaji wa CHADEMA imeelekezwa kwenye kampeni, kushinda uchaguzi huu kwa
ajili ya kuleta mabadiliko ambayo Watanzania wanayahitaji sana, wanayaunga
mkono na wako tayari kuyapigia kura hapo Oktoba 25, kwa sababu wakati wake ni
huu.
Wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA
wakishirikiana na wenzao wa vyama vinavyounda UKAWA, wanaendelea kujikita
katika mikakati ya kutafuta ushindi wa Mgombea Urais, Edward Lowassa akiwa na
Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji halikadhalika wabunge na madiwani nchi nzima.
Imetolewa
leo Jumatano, Agosti 2, 2015 na;
Tumaini
Makene
Mkuu wa
Idara ya Habari na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment