MGOMBEA
ubunge jimbo la Temeke,kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Abbas Mtemvu
amekemea vikali viongozi wa chama hicho wanadharau wananchi baada ya
kuchaguliwa kwakuwa wananchi ndiyo wenye mamlaka sahihi.Hayo yalisemwa
na Mbunge huyo alipokuwa
akizindua
rasmi kampeni yake ya jimbo hilo,ambayo ilihudhuriwa na wananchi zaidi
ya 600 wenye mapenzi ya mgombea huyo,huku akisindikizwa na viongozi wa
Chama hicho akiwemo Katibu Mwenezi wa Mkoa Juma Simba,Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Temeke Yahaya Sikunjema,na Madiwani wateule kama Noel
Kipangule wa Chang'ombe,Francs Mtawa wa keko.
Alisema
kuwa hawezi kunyama na kuvumilia mfumu wa baadhi ya viongozi kudharau
wananchi wao baada ya kuchaguliwa kwakuwa wao sio wenye mamlaka ya
kujichagua bali ni wananchi.
Alisema
kuwa inasikitisha mno kuona wagombea wanakuja mikono nyuma kabla ya
kupata lakini wanakuwa miungu watu baada ya kushinda. |
No comments:
Post a Comment