Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
leo wameibuka na kudai kuwa sasa ni miezi motano hawajui wala kuonja ladha ya
mshahara huku kukiwa hakuna maelekezo wala kauli yoyote kutoka serikalini jambo
ambalo limezua taharuki kubwa ndani ya mamlaka hiyo na kusababisha wafanyakazi
wa shirika hilo kukutana kujadili hali hiyo inayowakumba.
Mtandao huu umekutana
na mkutano uliokuwa unafanyika ndani ya mamlaka hoyo ulioitishwa na chama cha
wafanyakazi wa reli nchini Tanzania TRAWU kikiwashirikisha wafanyakazi wote wa mamlaka
hiyo ambapo mada kuu katika mkutano huo ni kujadili hali ngumu waliyonayo
ambapo wamesema kuwa hadi sasa ni mwezi
wa tano hawajapata mishahara yao huku wakiwa wamelalamika serikalini bila
majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa chama
hicho MUSA KALALA amezungumza na mtandao huu kuhusu madhumuni ya mkutano huo
ambapo amesema kuwa lengo lao sasa ni kupaza sauti yao kuhusu mishahara ili serikali iweze kuwasikiliza na kuwasaidia.
Bwana MUSA amesema kuwa
huu ukiwa ni wakati wa uchaguzi ni lazima serikali itambue kuwa wafanyakazi wa
shirika hilo ni wapiga kura,na wanawahudumia wapiga kura hivyo kuwanyima haki
yao kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo makubwa kuelekea uchaguzi mkuu
wa mwaka huu.
Ameongeza kuwa kumekuwa
na matatizo makubwa yanayowakumba wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja
na wengine kufukuzwa kazi au kusimamishwa kutokana na kuonekana wanadai haki
yao kwa kasi mbele ya jamii jambo ambalo amesema sasa uongozi wa chama hicho unaliangalia
ili waliofukuzwa waweze kurejea kazini mara moja.
No comments:
Post a Comment