Meneja wa HEINEKEN nchini Tanzania Bwana Michael Mbungu akizungumza na
mtandaso huu wakati wa Tamasha hilo alisema kuwa Bia yao inajivunia sana kuwa
moja katimya wadhamini wa Tamasha kubwa kama hilo nchini huku akisema kuwa
udhamini wa matukio mbalimbali ni moja wa mkakati wao wa masoko ili kuendelea
kuwa na ushirikiano wa karibu sana na wadau ambao ndio wateja wao wa kila siku.
Alisema kuwa moja ya
sababu kubwa iliyowavutia wao kama HEINEKEN kuweka udhamini wao katika Tamasha
la NYAMA CHOMA FESTIVAL ni kutokana na ubora na umakini wa tamasha hilo pamoja
na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa Kiongozi na mwanzilishi na
Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo,Carol Ndosi ambapo amesea kuwa lengo kuu ni
kuleta starehe kwa watanzania kwa njia ya kuwajibika
Wadau na wapenzi wa Kinywaji cha HEINEKEN waliokuwa wanaendelea kupata burudani ya aina yake katika viwanja hivyo. |
Aidha mkurugenzi mtendaji wa Alta Vista Events Carol Ndosi akizungumza
na mtandao huu amesema kuwa moja ya mikakati ya Tamasha hilo Tangu kuanzishwa
kwake ni kuhakikisha kuwa linavuka nje ya Tanzania na kufika katika nchi za Africa
mashariki ambapo amesema kuwa mkakati huo unaendelea kufanyiwa kazi.
Alisema kuwa Tamasha hilo limekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa
kwake ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuleta watanzania wengi pamoja na kuwa na
mapenzi na nyama choma na kuendelea kutoa Burudani mbalimbali kwa watanzania
ambao wamekuwa wakihudhuria Tamasha hilo
Bend maarufu ya FM ACADEMIA wakitoa burudani viwanjani hapo. |
No comments:
Post a Comment