Baadhi ya madawa na vipodozi ambavyo vimekatwa katika operation hiyo |
Mamlaka ya chakula na
dawa nchini Tanzania TFDA kwa kushirikiana na jeshi la polisi na shirikisho la
polisi kimataifa INTERPOL wamefanikisha kukamatwa kwa dawa na vipodozi haramu
vyenye thamani ya shilingi million 135,994,950 .
Ukamatwaji wa dawa hizo
na vipodozi haramu ni matokeo ya operation Giboia 2 yenye lengo la
kubaini,kukamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaojihusisha na
biashara dawa bandia,dawa za serikali,dawa ambazo hazijasajiliwa,dawa duni,dawa
zilizoisha muda wa matumizi,vipodozi ambavyo havijasajiliwa na vipodozi ambavyo
vina viambata sumu.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo HIITI SILLO akizngumza na wahabari leo |
Akizungumza leo Jijini
Dar es salaam na wanahabari kaimu kamishna wa jeshi la polisi mkoa wa Dar es
salaam HEZRON GYIMBI ameeleza kuwa maeneo
243 yalikaguliwa wakati wa operation hiyo ikiwa ni maeneo 115 ya Dar es
salaam,17 mtwara,13 kilimanjaro,12 arusha,18 mwanza,27 mbeya,na 32 dodoma
ikiwahusisha waingizaji wa madawa famasi
za jumla na reja reja,maeneo ya hospitalini,vituo vya afya,maduka ya dawa
muhimu pamoja na maduka ya reja reja na jumla ya vipodozi.
Kaimu kamishna wa jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam HEZRON GYIMBI akizngumza na wanahabari mapema leo juu ya zoezi hilo la operaration GIBOIA 2 |
Kwa upande wa mamlaka
ya chakula na dawa TFDA Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo HIITI SILLO amesema kuwa kufanyika kwa operation
GIBOIA awamu ya pili ni makubaliano ya mkutano uliofanyika tarehe 9-10 April
mwaka huu Harare ili kupiga vita bidhaa bandia na utekelezaji wa maazimio
ambayo yalifikiwa katika mkutano huo uliowashirikisha pia shirika la kimataifa la polisi INTERPOL pamoja
na shirika la afya duniani WHO kwa nchi nane zilizopo kusini mwa jangwa la
sahara ambazo ni Africa kusini,Zimbabwe,Malawi,Msumbiji,Swazland,Zambia,Angola
na Tanzania kwa muda wa siku tatu zoezi ambalo lilifanyika kwa muda wa siku
tatu tarehe 19-21Augost 2015.
Wanahabari mbalimbali wakiwa katika kkutano wa utangazaji wa matokeo ya Operation hiyo |
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa tanzania TFDA, HIITI SILLO akimuonyesha kaimu kamishna wa polisi Sample ya bidhaa haramu ambazo zimefanikiwa kukamatwa katika zoezi hilo nchini.PICHA ZOTE NA EXAUD MSAKA HABARI |
Amesema kuwa kutokana
na matokeo ya zoezi hilo hatua mbalimbali zitachukuliwa dhidi ya watu waliokamatwa
na makosa hayo ambapo hadi sasa amesema kuwa jumla ya majalada 19 ya kesi
yamefunguliwa katika vituo mbalimbali vya
polisi nchini dhidi ya watuhumiwa
No comments:
Post a Comment