Monday, September 14, 2015

MALINZI AZINDUA KAMBI YA U13


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo amezindua rasmi kambi ya kikosi cha timu ya Taifa umri chini ya miaka 13 ambacho kitakua pamoja kuelekea fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17  (U17) zitakazofanyika nchini Tanzania mwaka 2019.

Kikosi hicho ni cha vijana 20 ambao waliteuliwa tokana na mashindano ya vijana ya umri chini ya miaka 13 (U13) yaliyofanyika Mwanza mwezi Juni mwaka huu.
Malinzi amezindua kambi hiyo itakayodumu kwa muda wa miaka mitano hadi mwaka 2019. Kambi hiyo itakuwa  kwenye shule ya kulea na kukuza vipaji vya mpira ya Alliance iliyopo jijini Mwanza.
Wakiwa Alliance vijana hao gharama za masomo, matunzo na vifaa zitatolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Akizindua kambi hiyo Malinzi aliongea na wazazi wa watoto hao na kuwaahidi kuwa TFF kwa kushirikiana na shule ya Alliance itahakikisha vijana hao wanapewa elimu nzuri itakayozingatia maadili.
Wazazi wa watoto wametoa shukrani kwa uteuzi huu wa watoto wao na Mkurugenzi wa shule ya Alliance Bw James Bwire ameahidi kutoa elimu bora na mafunzo mazuri kwa vijana.
Jumla ya vijana 455 toka mikoa yote ya Tanzania walishiriki mashindano hayo

No comments: