Saturday, October 24, 2015

Picha 80---LOWASA AISIMAMISHA DAR KWA SIKU NZIMA

Hapa kuna picha zaidi ya 60 za kwanza nilizokukusanyia kutika katika mkutano wa kufumga wa kampeni wa UKAWA katika viwanja vya jangwani,unaweza kutizama kila kitu kilichojiri hapo kwa mfumo wa picha na kushare na wengine pia.





Umati mkubwa wa watanzania na wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza kumsikiliza mgombea huyo.
HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA JANGWANI OKTOBA 24, 2015
NDUGU
Watanzania wenzangu

? Ndugu

wanachama, marafiki na wapenzi wa CHADEMA
? Ndugu
Viongozi wakuu wa kitaifa na wanachama wa vyama vyetu vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
? Ndugu
Wana mabadiliko na watetezi wa kweli wa maendeleo
? Mabibi kwa Mabwana

Salaam Aleikum
Bwana Yesu Asifiwe
Tumsifu Yesu Kristo
NIANZE hotuba yangu hii ya kuhitimisha ziara ndefu za kampeni, zilizonichukua mimi na timu yetu yote ya kampeni katika kaya, vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar katika kipindi chote cha siku takriban 60.

Kama nilivyosema jana nilipozungumza na Watanzania kupitia katika redio, televisheni na kwa njia tofauti za mawasiliano, tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetuvusha salama.

Leo tunahitimisha safari ngumu, ndefu, iliyojaa miiba, milima na mabonde tukitembea kifua mbele kwa namna mamilioni ya Watanzania walivyojitokeza kutuunga mkono.
Kwa uchungu na masikitiko makubwa tunahitimisha safari ya kampeni, tukiwa na kumbukumbu mbichi vichwani ya kuwapoteza wenzetu kadhaa.

Ni juzi tu, wiki hii hii tumemlaza katika nyumba yake ya milele Mzee wetu, Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Emmanuel Makaidi.
Tumewapoteza njiani kabla yake, Deo Filikunjombe, Dk. Abdallah Kigoda, Mama Celina Kombani, kijana wetu Mohamed Mtoi na Estom Mallah, wote hawa walikuwa wagombea ubunge.

Si hao tu, tukampoteza pia mmoja wa wanasiasa ambaye ni muasisi wa mageuzi nchini, Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.
Wote hao na wengine ambao sikuwataja hapa tunamuomba Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani. (Tusimame dakika moja kuwakumbuka marehemu wote waliopoteza maisha katika kipindi hiki cha kampeni)
Ndugu zangu

Mimi na mgombea mwenza, Juma Haji Duni tumeona na kujifunza mengi. Tumejiandaa kikamilifu kuijenga Tanzania Mpya. Tanzania ya ndoto ya waasisi wetu.
Ndugu Watanzania wenzangu

Katika ziara hizi, nimeshuhudia vuguvugu la mabadiliko, kiu na ari ya Watanzania kuyapokea mabadiliko hayo.

Lakini pia nimejionea shida zinazowakabili wananchi hao.
Nimesikia na nyakati nyingine kujionea kilio chao cha kunyanyaswa na kunyimwa haki zao na watendaji wa serikali na baadhi ya vyombo vya dola.


Nimekisikia kilio chao cha umaskini, afya na elimu duni.

Nimekisikia kilio kikubwa cha vijana kukosa ajira na matarajio ya kesho bora.
Nimesikia rai za Watanzania na ndoto zao za kupata maendeleo, maji safi, makazi bora na barabara madhubuti.
Nimesikia malalamiko ya wakulima na wafugaji kukosa maji, ardhi na namna wanavyotozwa ushuru na kodi za kero katika mazao yao.

Nimesikia kilio cha madaktari, wauguzi, walimu, askari na watumishi wa taasisi za umma kuhusu mazingira magumu ya kazi, kodi za juu na maslahi duni.
Nimesikia kilio cha wafanyabiashara wadogo wadogo kuhusu ugumu wa mazingira ya kufanyia shughuli zao, kodi kandamizi na kukosa mitaji.

Nimesikia kilio cha wanawake kuhusu haki zao na ushiriki wao mdogo katika shughuli za kiuchumi.
Nimesikia kilio cha wazee na wastaafu wasio na bima ya afya, wanaolipwa pensheni isiyokidhi mahitaji yao na ugumu wa maisha yao uzeeni.

Tumekisikia kilio dhidi ya rushwa na ufisadi uliokithiri
Tumekisikia kilicho cha Watanzania juu ya udhaifu wa kiuongozi na utawala dhaifu wa CCM ulioshindwa kuondoa umaskini
Tumekutana na vilio vya watu walioonewa, kunyanyaswa na kupuuzwa na namna haki za raia zilivyopuuzwa.
Jibu langu ni fupi na lile lile. TUMEONA, TUMESIKIA, TUMEELEWA NA TUTATENDA.

Baba wa Taifa, alisema Uongozi ni kuonyesha njia. Tumejipanga vyema kuwaongoza Watanzania:
? Kwanza tumejiandaa kuongoza mapambano ya dhati ya kuukataa na kuondokana na umaskini
? Tumejipanga vyema kupiga vita rushwa na ufisadi kwa matendo na si kwa maneno matupu
? Tumejizatiti kuliandaa taifa kwa ajili ya mapinduzi ya kweli katika elimu, kilimo, viwanda
? Tumejiandaa vyema kuwaongoza Watanzania kuachana na mawazo ya kutegemea wafadhili na kuondokana na hulka za kuwa taifa ombaomba
? Tumejipanga kufufua ari, dhamira na misingi ya kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi.




































































No comments: