Wenyeviti wa umoja wa
katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha democrasia na
maendeleo chadema ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Hai pamoja na mwenyekiti
wa NCCR mageuzi ambaye poa ni mbunge mteule wa jimbo la vunjo pamoja na makamu
mwenyekiti wa cha cha democrasia na maendleo chadema Profesa ABDALA SAFARI
jioni ya leo wamezungumza na wanahabari kuhusu maswala mbalimbali aambayo
yanajitokeza kipindi hiki cha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania,Hapa
nimejaribu kukunukulia baadhi ya maswala muhimu ambayo wamezunguzia hapo.-------------
MBOWE---Huu haukuwa
uchaguzu ulikuwa ni uchafuzi na vita kubwa sana,haukuwa uchaguzi wa huru na
haki.
MBOWE—Kwanini majimbo
ambayo wagombea wetu wameshinda inakuwa ni vigumu sana kwa matokeo kutangazwa
hadi itokee mabomu na nguzu kubwa sana ndipo matokeo yatangazwe,pilisi
wanajaribu kulazimisha matokeo ambayo wanayajua wao wakishirikiana na wakuu wa
wilaya na wakuu wa mikoa ambao wote wanajaribu kukisaidia chama cha mapinduzi.
MBOWE—Hatuyatambui wala
kuyapokea matokeo ambayo yanatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu kura
za urais kutoka katika majimbo mbalimbali,matokeo hayo hayaendeni hata kidogo
na ukweli wa mambo na wala hayafanani hata kidogo na Form ambazo sisi tunazo
kutoka kwa mawakala wetu hatuyataki.
MBOWE—Vijana wetu na
wataalamu wa IT ambao walikuwa wanafanya kazi halali kabisa ya kiukisaidia
chama kupata matokeo kutoka kwa mawakala wetu kote nchini na kuyajumlisha ili
wawee kulinganisha na matokeo ambayo yanatolewa na tume,wamekatwa toka juzi
vijana zaidi ya 160,wamevamia center yao,wameharibu mifumo yao ya upokeaji wa
kura na kuvunja baadhi ya vifaa vyetu vya kufanyia kazi hiyo.
MBOWE—Wamewagawanya vijana
hao katika vituo mbalimbali vya polisi wengine jana wamepelekwa segerea kukaa
huko na tumepata taarifa kuwa vijana wengine walikuwa wanapelekwa mahakama ya
kisutu jioni hii na tumefika pale ni kweli vijana wetu nane wamefikishwa pale
na wamefunguliwa mastaka ya makosa ya mtandaoni jambo ambalo ni lakushangaza
kweli.
MBOWE—Hii sio haki
kwani vijana hao walikuwa wanafanya kazi halali kabisa,wakati huo huo CCM wao
vijana wao ambao wapo HYJAT HOLEL jijini Dar es salaam na tunajua wapo
wanafanya kazi hiyo hiyo na JANUARY MAKAMBA kila siku anatangaza matokeo
wanayopokea ila wao wanaonekana hawana kosa lolote ila wakifanya ukawa ni CYBER
CRIME.
MBOWE—Kwa misingi hiyo
sasa tumeamua kuwa,kesho tukutane kamati kuu ya chadema ikiwa ni kamati kuu ya
dharura kujadili nankuamua nini kifanyike baada ya uchaguzi huu kuharibika wazi
wazi,na kesho hiyo hiyo pia tutakutana summit ya viongozi wakuu wa vyama vya
UKAWA kujadili na kutoa maamuzi ya maswala haya.
MBATIA—Huu sio uchaguzi
ni vita kubwa sana,kwa mfano juzi kule vunjo Kilimanjaro nililala nje tukipita
kukusanya masanduku yaliyokuwa yamefichwa majumbani mwa watu yakiwa na kura za
Rais wa CCM na tukakamata mengi sana ila tumepeleka polisi baadae wakakanusha
na kusema kuwa hakuna jambo lililotokea bali ni masanduku ya tume yalikuwa yakipekewa katika vituo.
MBATIA—Lengo letu kama
ukawa ni kudumisha amani ya Tanzania,tunafanya haya yote ili kuokoa taifa hili
lisije likaingia katika machafuko ya aina yoyote.
MBATIA—Namaliza kwa
kusema hivi unaweza kuchakachua kura ila huwezi kuchakachua hisia za
watanzania.Asanteni
Katika tamko lake, Profesa Safari ametolea mfano jimbo la tandahimba ambapo amesema, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo,Magufuli amepewa kura 49,098 huku Lowassa akiambulia 46,288
Kwa mujibu wa Profesa Safari, matokeo halisi waliyoyakusanya toka kwa mawakala wao yanaonyesha kuwa Magufuli ana kura 44,253 huku Lowassa akiwa na kura 44,537
No comments:
Post a Comment