Friday, October 23, 2015

WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA AMANI KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI

Waislam wa dhehebu la SHIA leo Wameanza maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa mtume IMAM HUSSEN ambaye alikuwa mtetezi wa haki za binadamu,utu na mpenzi wa amani Duniani,maadhimisho ambayo waislam hao wameyatumia kutoa ujumbe wa kulinda na kutunza amani ya Tanzania hususani kupindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Akizngumza na mtandao huu wakati wa mataemebezi ya amani ya kuadhimisha kifo cha mpenda amani huyo Kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA amesema kuwa IMAM HUSEIN ni moja kati ya watu waliopoigania sana uwanadamu na utu duniani na alikuwa anaienzi amani ya dunia na kuhamasisha amani katika mataifa ambayo yalikuwa yakiyumba kiamani.

Amesema kuwa watanzania ni muda wa kutumia maadhimisho hayo kuenzi amani tuiyonayo watanzania kipindi hiki cha uchaguzi na kuhakikisha kuwa tunapiga kura na kupata viongozi wanaoweza kulisaidia taifa hili.

SHEIK JALALA pia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kapiga kura hapo siku ya Jumapili.
PICHA ZA MATEMBEZI HAYO ZIPO CHINI-----------


No comments: