JESHI la Polisi nchini limepiga marufuku mikutano yote ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema iliyotarajiwa kufanyika kesho kutwa Jumapili nchi nzima.
Akitoa katazo hilo, leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini,Advera Bulimba ambapo amesema Jeshi la Polisi limepata barua kutoka kwa Chadema iliyokuwa inataka kuomba ruhusa ya kufanyika kwa mkutano kila mkoa ambao ulitakiwa kufanyika jumapili wenye lengo la kutoa sera kwa wananchama wake.
Bulimba amesema mara baada ya Jeshi hilo kupata barua hiyo wakafanya Tasmini na kubaini bado nchini kuhali tata ya usalama.
“Tumekata mikutano hii,baada ya kubaini kuna mihemuko ya kisiasa ndani ya jamii yetu,hivyo mikutano au maandamano ya aina hiyo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani endapo ikutuhusiwa”amesema Bulimba.
Ameongeza kuwa “Jeshi la Polisi bado linasisitiza katazo lake la awali liliozuia mikutano na maandamano mpaka hapo hali itakapotengamaa”
Hata hivyo,Jeshi hilo la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote nchini kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha uchaguzi kwa kujiepusha na vitendo vyovyote vitavyoleta uvunjifu wa amani
No comments:
Post a Comment