Friday, November 6, 2015

Breaking newzz--Picha ya Rais MAGUFULI yapigwa stop kutumika Muda huu

Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma  na  wananchi  kwa ujumla  kwamba  imesitisha    matumizi  ya  picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John Joseph Pombe Magufuli mpaka  hapo itakapotangazwa tena.

Awali  majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi  ya  picha ya Rais, ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa gharama ya Shilingi Elfu Kumi na Tano tu (15,000/=).
Aidha,   Serikali  imesema kwamba  itazitangazia  ofisi hizo na umma wa Watanzania  kuhusu kuanza tena kwa  matumizi ya picha  hiyo hapo baadae.
Imetolewa na
IDARA YA HABARI.
Novemba 6,mwaka 2015

No comments: