Tuesday, November 3, 2015

RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA MBETTE KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA


RAIS WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA 

TAARIFA
KWA UMMA 

UTEUZI
WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA 

        Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette  kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha
miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015.  

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu
Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili
2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. 

Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria,
TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya
Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London,
Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. Pia ameshirikiana
na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika
katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida
mbali mbali. 

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia

No comments: