Wafanyakazi wa kituo
cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC ambao walikuwa wanafanya
uangalizi wa uchaguzi kupitia mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi
nchini TACCEO wameendelea kusota polisi baada ya leo kufanyiwa mahojiano ya awamu
ya pili kuhusu tuhuma mbalimbali zinazowakabili.
Wafayakazi hao wapatao
38 walikamatwa na jeshi la polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu nchini
huku vifaa vyao pia vikikamatwa kwa tuhuma za kusambaza habari za uchaguzi mkuu
kinyume na sheria za uchaguzi na katiba ya Tanzania.
Akizungumza na
wanahabar ndani ya makao makuu ya polisi nchini Kamishna wa polisi kanda maalum
ya Dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwahoji
wafanyakazi hao 38 wa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa tuhuma za
kukusanya na kusambaza taarifa zisizo sahihi kwenye mitandao ya kijamii kinyume
na kifungu namba 16 cha sheria inayodhibiti makosa ya kimtandao.
Kamishna KOVA amesema
kuwa wakati wa harakati za kusubiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi
karibuni zilipatikana taarifa za kuaminika kuwa kituo hicho kilikuwa
kinajihusisha na upokeaji wa matokeo kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura
kutoka kwa mawakala wao waliowaweka nchi nzima na hatimaye kusambaza taarifa
hizo kwa watu wasiohusika ikiwemo mitandao ya kijamii ambapo amesema kuwa
kisheria kazi ya kupokea na kusambaza matokeo ni ya tume ya taifa ya uchaguzi
pekee.
Amesema katika mahojiano
ya awali polisi waligundua kuwa kituo hicho kilipewa kibali na tume ya taifa ya
uchaguzi kuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi ambapo walipewa masharti ya namna
ya kuendesha kazi zao ikiwa ni pamoja na kutotoa maoni na taarifa yoyote kwa
vyombo vya habari au umma juu ya mchakato wa uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga
kura likiendelea au kutofanya majukumu ya kiutendaji ya tume ya taifa ya
uchaguzi chini ya kifungu namba 12 cha maelekezo kwa waangalizi wa ndani na
wanje wa uchaguzi 2015.
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA akizungumza na wanahabari nkuhusu sakata hilo |
Amesema kuwa polisi
wamegundua kuwa wamekuwa wakikiuka masharti na sheria hizo hivyo wamewaita ili
kuweza kuwafanyia mahojiano zaidi ili wakipatikana na hatia sheria iweze
kuchukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na kupeleka jalada hilo kwa mwanasheria mkuu wa serikali na kama
kuna wengiune watakutwa hawana hatia wataachiwa huru wao pamoja na vifaa vyao
LHRC WAZUNGUMZA.
Akizungumza na
wanahabari nje ya makao makuu ya polisi mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria
na haki za binadamu HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa baada ya wafanyakazi wao kufanyiwa
mahijiano ya mara ya kwanza leo wameitwa tena kwa ajili mahojiano ya nyongeza
juu ya sakata hilo hivyo vijana wake wameitika wito huo.
Amesema kuwa kituo
chake kimeathirika sana na tukio hilo kwani limefanya kazi za wanaharakati hao
zimesimama kwa muda usiojulikana huku vifaa na vitendea kazi vyao vikiwa
vimeshikiliwa na jeshi la polisi huku wakiwa hawajui hatma ya sakata hilo kwa
ujumla.
Tukio la kukamatwa kwa
wafanyakazi wa kituo hicho ni tukio la pili baada ya tukio la kwanza
lililotokea huko njombe kipindi cha uandikishwaji wa BVR ambapo Bi HELLEN KIJO
BISIMBA amesema haelewi ni tatizo gani linawakumba kwani wanafanya kazi kwa
mujibu wa shetia na wakiwa na vibali vyote vya kufanya kazi za uangalizi.
No comments:
Post a Comment