Friday, November 6, 2015

Rais Dkt.Magufuli amwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Dar leo

01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimina na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati aliwapowasili kwenye Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Okt. 6, 2015 kwa ajili ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, aliyemteua jana Okt 5, 2015 mara tu baada ya kuapishwa rasmi. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande. (Picha na OMR)
02
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Okt. 6, 2015.
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiwa na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, baada ya kuapishwa leo wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, (kushoto) akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (katikati)  wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
3
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki na watumishi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. (Picha na OMR).
Dewji Blog 

No comments: