Aliyekuwa
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa miaka nane katika awamu
iliyopita Ludovick Utouh ameibuka na kuipongeza kasi aliyoanza nayo Rais wa awamu ya
tano Mh JOHN MAGUFULI huku akisema kuwa kasi hiyo inahitaji msaada kutoka kwa
watendaji wa chini kwani Rais hana uwezo wa kushughulikia kila wizara bila
msaada wa watendaji wenye moyo wa kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Wakili EMELDA LULU URIO akizungumza katika hafla hiyo |
Mh Ludovick Utouh
katika hafla ya kumkabidhi tuzo kiongozi huyo iliyotolewa na Kituo cha sheria
na haki za binadamu nchini LHRC tuzo inayoitwa Tuzo ya maji maji,tuzo ambayo
inatolewa kila mwaka kwa mtu au kiongozi ambaye katika utendaji wake
amejipambanua kulinda haki za binadamu pamoja na kutetea utawala bora,tuzo
ambayo kwa mwaka huu ni mara ya tatu kutolewa na kwenda kwa mdhibiti huyo na
mkaguzi wa hesabu za serikali mstaafu Ludovick
Utouh
Mchapalo ukiendelea |
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo Utouh alisema kuwa ni furaha kuona kazi
aliyoifanya inatambuliwa na watu na mashirika mbalimbali na kuamua kumpongeza
jambo ambalo amesema kuwa ni furaha kwake na kuona kuwa kazi aliyoifanya ni
msada kwa watanzania waliowengi.
Alisema
kuwa wakati wa utendaji wake aliamua kusimamia ukweli na haki hasa katika
maswala ya ufisadi na matumizi mabaya ya Mali za watanzania ambapo wakati
mwingine alionekana kama hana nia njema na serikali yake lakini hiyo ndiyo
iliyompa heshima katika nafasi hiyo.
Wafanyakazi wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu nchini Wakiongozwa na Kaimu mwenyekiti wa kituo hicho EMELDA LULU URIO wakiwa wamebeba Tuzo hiyo ambayo ilinyakuliwa na LUDOVICK UTOUH. |
Akizungumzia
uamuzi wa Rais MAGUFULI wa kuwaondoa wabunge wote katika bodi za mashirika ya
UMMA amesema kuwa hilo ni jambo lililokuwa linamshangaza sana katika seikali ya
awamu ya Tano kwani ilikuwa haileti maana mbunge ambaye anatakiwa kuihoji
serikali na kuisimamia anakuwa ni mmoja kati ya wanaonufaika na serikali hiyo jambo
ambalo liliwafanya wabunge wengi kushindwa kuhoji maswala nyeti ya serikali kwa
kulinda maslahi yao.
Mazungumzo ni sehemu ya Furaha |
“Nilikuwa
kila siku nadai hili swala la wabunge kuwepo katika Bodi za mashirika ya
UMMA,hadi nilionekana kama mtu mbaya sana,ila nilichokuwa nasimamia
niliakiamini,nashukuru sana kwa Rais Mpya kuamua kufanya hivyo kwani itawafanya
wabunge sasa kuwa huru kuihoji serikali katika maswala nyeti na makubwa”Alisema
Ludovick Utouh
Alitolea
mfano sakata la ukwapuaji wa fedha za ESCROW lilivyokuwa linajadiliwa bungeni
akasema kuwa kuna baadhi ya wabunge walikuwa hata hawaelewi waongee
nini,wengine ukiwasikia hujui hata wanaongea nini,wengine walikaa kimya yote
kwa sababu swala hilo na wao wapo katika mashirika hayo,ila sasa naamini kuwa
serikali nitakwenda.
No comments:
Post a Comment