Meya mpya manispaa ya Temeke Mh ABDALAH UREMBO akizngumza na wanahabari nje ya Mkutano huo |
Katibu Tarafa wilaya ya Temeke Mh LAWRENCE MALANGWA amewataka
madiwani wa manispaa hiyo kuwa wabunifu katika kupanua vyanzo vya mapato
mbalimbali katika manispaa hiyo.
Akizungumzia hilo leo jijini Dar es salaam wakati nwa
uapishaji wa madiwani wa manispaa hiyo ya temeke LAWRENCE MALANGWA amesema kuwa
ni vyema madiwani hao wakatumia fursa na ubunifu walionao katika kupanua vyanzo
mbalimbali vya mapato ya manispaa hiyo na kuacha kuonea wafanya biashara wadogo
wadogo katika ukusanyaji wa kodi huku
akisema kuwa wananchi wanategemea kufanya shughuli zao bila ya kusumbuliwa
katika biashara zao ili waweze kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya madiwani wa Temeke wakila kiapo |
Aidha meya mya
manispaa hiyo Mh ABDALAH UREMBO amewataka madiwani kutekeleza sera
walizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni na pia kuwa na hofu ya mungu katika kuwatumikia wananchi kwani wananchi wa
leo sio wa jana wa sasa ni wafwatiliaji na wana maamuzi ya hapo kwa hapo pale
wanapoona unawatendea kinyume na matakwa yao,pia amewataka madiwani wote kumpa
ushirikiano bila kujali itikadi za kisiasa ili kupeleka Gurudumu la maendeleo
mbele
Madiwani wakisikiliza kwa makini |
No comments:
Post a Comment