Kampuni ya
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Reach for Change (R4C) wametangaza washiriki 15 wenye vipaji vya ujasiriamali wa
kijamii wamechaguliwa katika shindano la “Tigo Digital Change Makers’ ambapo washindi
wawili watatangazwa wiki ijayo.
Shindano hili lilioanza Septemba,
limepokea mamia ya maombi kutoka kwa washiriki wenye ubunifu wa kiteknologia katika
sekta mbalimbali zikiwemo elimu, ukulima na afya kwa mujibu wa Afisa wa Huduma
kwa Jamii wa Tigo, May Thomas
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo
vya habari jijini Dar es Salam leo, May amesema, wajasiriamali wa kidijitali 15
waliochaguliwa kila mmoja wao alileta
suluhisho la kidijitali lenye ubunifu lilokusudia kuboresha maisha ya watoto
nchini Tanzania, na ndio kigezo kilicho wafanya wafuzu kushiriki katika
shindano hilo.
May alisema: wengi katika hawa
waombaji fikra zao ubunifu zimeenda sambamba na mkakati wetu wa kuleta
mabadiliko ya kidijitali maishani. Hali imesababisha changamoto kubwa katika zoezi
la kuchagua washindimda,” alisema, huku akiongeza kuwa washindi hao wawili
watapokea dola za
kimarekani 20,000 kila mmoja kwa ajili ya
kutekeleza miradi yao.
Tigo na Reach for Change wameendesha
shindano hili la Digital Change-Makers nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka
mitatu sasa, ambapo wajasiriamila wa kijamii
saba wameshinda fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi yao. Kwa mujibu wa
May, miradi ya wajasiriamali wa kijamii hao saba kwa pamoja imesaidia ya zaidi
ya watoto 10,000 nchini katika kipindi hicho.
Shindano la Tigo Digital –Makers lina
malengo ya kuwaendeleza na kuwatia moyo wajasiriamali wa kijamii kutumia teknolojia
za kidijitali kusuluhisha baadhi ya matatizo sugu nchini Tanzania
No comments:
Post a Comment