Wito umetolewa kwa watanzania pamoja na Serikali kuruhusu lugha
za asili kutumika kujieleza na kujitetea katika sehemu mbalimbali ikiwemo mahakamani.
Akizungmza katika
maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani iliyoandaliwa na kituo cha
sheria LHRC iliyofanyika katika uwanja wa makumbusho ya Taifa leo Jijini Dar es
Salaam,mwenyekiti wa tume ya kurtekebisha sheria nchini Tanzania ,Jaji Aloyce
Mjulia amesema kuwa watu wengi wanahukumiwa kwa kushindwa kujieleza.
Mwanasheria Harold Sungusia kutoka LHRC akiwasilisha moja ya mada katika maadhimisho hayo |
Amesema endapo mtu atapewa fursa
ya kutumia lugha anayoifahamu kwa kina ataweza kujieleza na kupata haki ya
msingi.
“Mimi nina uzoefu kwa
kazi hizi mara nyingi hata askari wetu hawafuati masharti ya haki za binadamu
kwani wanapowakata watuhumiwa wanahoji maswali ambayo wanajua kwamba watajibiwa
wanavyopenda wao.,
“Vile vile mahakamani mtu anatakiwa kujitetea kwa kutumia lugha
ambayo anaijua kwa kina na awepo mtu wa kutafsiri lakini mara nyingi utakuta
hii inatokea pale tu anapokuwepo raia wa kigeni,”amesema Jaji Mjulia
Kwa upande wake Mwanasheria kutoka LHRC Bwana Harold Sungusia
amesema vitendo vya uvunjifu wa Haki za binadamu nchini vimeongezeka sana huku
akitolea mfano kipindi kilichomalizika cha uchaguzi mkuu kwa kusema vyombo vya
dola hususani polisi wamekuwa ni watu wakutekeleza vitendo vya kinyama kwa raia.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC EMELDA LULU URIO akizungumza katika maadhimisho hayo |
“Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vimeongezeka sana
hapa nchini tumeshuhudia hata kipindi cha uchaguzi,maana hata sisi haki za
binadamu tumekuwa waathirika wa kubwa,vifaa vyetu vya uangalizi mpaka leo vipo
polisi,”amesem Sungusia..ENDELEA KUFAIDI PICHA ZA TUKIO NZIMA
No comments:
Post a Comment