Monday, December 7, 2015

Pichaz--Msanii KLEYAH alivyoitambulisha MSOBE MSOBE ndani ya TBC na FREE MEDIA.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania KLEYAH ambaye anatamba na wimbo wake mpya wa MSOBE MSOBE aliomtambulisha mwanamuziki BARNABA BOY ameendelea na ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari mbalimbali kutambulisha wimbo wake huo mpya ambapo katika safari hii amefanikiwa kufika katika kampuni ya magazeti ya FREE MEDIA ambao ni wazalishaji wa gazeti la TANZANIA DAIMA,Pichani ni msanii huyo akiwa na baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa kamouni hiyo mara baada ya kufanya mahojiano.


Msanii Kleyah katikati akiwa na mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Tanzania Daima SALUM MKANDEMBA  pamoja na LUCY NGONGOSEKE kutoka TABASAMU PR wakati wa ziara ya msanii huyo alipotembelea katika ofisi za FREE MEDIA.
Hapa ni TBC Taifa msanii kleyah akifanyiwa mahojiano na mtangazaji ENOCK BWIGANE kuhusu kazi zake za music
ENOCK BWIGANE na KLEYAH wakiwa TBC TAIFA

Msanii kleyah akiwa TBC ONE katika mahojiano


No comments: