Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali. Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia.
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika.
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika mashine za kawaida.
Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.
Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na CT-SCAN , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH, Dk Florah Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo yamekamilika na kwamba hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN .
Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 , Televisheni nne , Decoder 4 pamoja na Tv Stand 4.
Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni hiyo John Solomon ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo huduma za afya
No comments:
Post a Comment