Watanzania pamoja na
wakristo nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha kuwa wanaweka mbele na
kuzingatia amani ya Tanzania katika kipindi hiki cha sikukuu za krimas na mwaka
mpya kwani amani ya tannzania ndio msingi mkuu wa kuendelea kuijenga nchi yetu.
Wito huo umetolewa leo
Jijini Dar es salaam na mmoja kati ya viongozi wakuu wa kiroho wa waislam wa
dhehebu la shia Ithnasheriya nchini Tanzania ambaye pia ni kiongozi mkuu wa
chuo cha kiislam cha Imam swadiq Shekh HEMED JALALA wakati akitoa salamu za
Krismas kwa wakristo wote nchini pamoja na mwaka mpya kutoka kwa waislam hao mbele ya wanahabari Jijini Dar es salaam.
Akitoa salamu hizo za
Krismas kwa wakristo Shekh JALALA amesema kuwa wao kama waislam wanaamini kuwa
wakristo ni ndugu zao kwa misingi ya ubinadamu,ambapo amesema pia undugu huo
umejijenga zaidi kijamii na kitaifa hivyo ni jambo muhimu sana kutakiana kheri
kwani sikukuu hiyo ni watanzania wote bila kujali itikadi za kidini zilizopo.
Ameongeza kuwa wao kama
viongozi wa dini za kiislam wanaamini kuwa kukaa kwa pamoja,kujuana,na
kufanyiana wema ni msingi mkuu wa kuhakikisha kuwa jamii
inashikamana,inasikilizana,na inajijengea uwezo mkubwa wa kutatua changamoto zao
hasa za uvunjifu wa amani kwa jina la dini na itikadi ambapo amewasihi
watanzania kuhakikisha kuwa wanailinda amani ya Tanzania katika kipindi hiki
cha sikukuu.
Salamu hizo za sikukuu
kutoka kwa waislam hao pia zimeambatana na zawadi mbalimbali zikiwemo kadi na
zawadi nyingine kwa baadhi ya makanisa ikiwa ni njia ya kudumisha undugu uliopo
baina ya dini hizo mbili.
No comments:
Post a Comment