Aliyekuwa mgombea mwenza wa Urais Wa ukawa kupitia chama cha Democrasia na maendeleo Chadema JUMA HAJI DUNI maarufu kama Babu duni sasa ameanza kurejea kwenye chama chake cha zamani cha Cuf baada ya uchaguzi kumalizika mwaka jana.
Juma Duni alilazimika kuchukua kadi ya chadema ghafla ili aweze kuungana na mgombea wa Chadema EDWARD LOWASA katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka jana ambao John Pombe Magufuli aliiibuka kidedea.
Baada ya uchaguzi huo kumalizika kumekuwa na mijadala mingi ikijadili Je mgombea mweza Babu DUNI atarejea kwenye chama chake cha CUF ambapo alikuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho au ataendelea kuwa ndani ya CHADEMA.
Katika mkutano mkuu wa baraza la CUF lililokuwa linajadili hatma ya uchaguzi wa marudo zanzibar hapo jana mtandao huu ulifanikiwa kushughudia Babu duni akishiriki katika vikao hivyo kama picha zilivyonaswa hapo jambo ambalo linaloonyesha wazi kuwa DUNI amerejea ndani ya CUF.
Wanachama wa CUF waliopata nafasi ya kuzngumza na mtandao huu wameeleza kuwa DUNI hakuondoka CUF bali kilichotokea ni kupewa kadi ya chadema ili aweze kukidhi masharti ya kugombea nafasi ya Mgombea mweza na sasa amerejea ndani ya chama chake kama kawaida, CHINI KUNA PICHA KADHAA DUNI AKIWA MAKAO MAKUU YA CUF JANA |
No comments:
Post a Comment