Na Exaud mtei( Msaka
Habari)
Sakata la bunge la Tanzania
kutokurushwa moja kwa moja na shirika la habari Tanzania TBC limechukua sura mpya
baada ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kuibuka na kulaaani maamuzi
hayo huku ikiyaita ni kuminywa kwa democrasia na uhuru wa habari nchini Tanzania
na kuitaka serikali kuheshimu na kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa
inayojenga uhuru wa kujieleza kwa nchi wananchama.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo kaimu mkurugenzi wa kituo hicho IMELDA LULU URIO amesema
kuwa kusitishwa kwa matangazo ya bunge na chombo ambacho ni cha umma ni
kuonyesha dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuheshimu yaki ya kupata
habari ya kikatiba.
Amesema kuwa sababu
zilizotolewa na waziri mwenye dhamana ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh
NAPE NAUYE kuwa kusitishwa kwa matangazo hayo kunalenga kupunguza gharama za
uendeshaji ni sababu ambazo zinaleta maswali kuwa gharama hizi ni za nini?,na
kwa ajili ya nini?na zikitumika ni kwa manufaa ya nani?,na mchangiaji wa
gharama hizi ni nani?huku akisema kuwa TBC ni chombo cha Umma hivyo
kunawajibika kwa wananchi wote bila kujali gharama.
Ameongeza kuwa Tanzania
ni moja kati ya nchi ambazo zimesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa
inayohakikisha upatikanaji wa taarifa ikiwa ni pamoja na ule wa OPG –Open government
partnership ambao ni jukwaa la serikali zenye uwazi mkataba ambao una misingi
ya uwepo wa uwazi,ushiriki,wa wananchi,uwajibikajina uweledi na ubunifu wa
kutumia Tehama.
Waandishi wa Habari wakipata Habari |
Amesema kuwa LHRC
inaitaka serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio ya makubaliano ya kimataifa
na kikanda katika kulinda haki ya kupata habari na kufuta sheria kandamizi
zenye kuminya uhuru huu kwa mfano sheria ya magazeti na sheria ya makosa ya
mitandao na kutunga sheria wezeshi.
Pia LHRC wameitaka
serikali kuacha kuminya haki za watanzania ya kupata habari za bunge kwa
kisingizio cha gharama,na kutenga rasilimalin nyingi kuwezesha shirika hilo
waweze kuonyesha moja kwa moja matangazo ya bunge.
Tangazo la
kutokuonyeshwa kwa bunge kupitia TBC lilitolewa bungeni na waziri wa Habari
NAPE NAUYE na baadae jana waziri mkuu Mh KHASIM MAJALIWA alitoa msisitizo kuwa
wameamua kusitisha matangazo hayo kutokana na kupunguza gharama za uendeshaji
No comments:
Post a Comment