Friday, January 29, 2016

BAWATA WAUNGA MKONO TAMKO LA SERIKALI

WMkurugenzi wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.
Picha na Beatrice Lyimo
…………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho-Maelezo
Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.
“kwa niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.
Ameongeza kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na  kupendekeza  zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.
Tamko hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa tiba za  asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu afya ya jami

No comments: