Tuesday, January 12, 2016

MAJALIWA AMPA POLE MAMA MARIA NYERERE

LE1
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitia saini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa zamani,Leticia mageni Nyerere wakati alipokwenda kumhani mjane wa Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es salaam Januari 12, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
LE2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa neno la faraja kwa Mjane wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere (kulia) wakati alipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa, Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa Mbunge wa zamani Leticia Nyerere. Kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LE3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (wapili kulia) wakiifariji familia ya Mjane wa Baba waTaifa, Mama Maria Nyerere (kulia) wakati walipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa mbunge wa zamani, Leticia Nyerere, Januari 12, 2016. Kushoto ni mtoto wa baba wa Taifa, Rose Nyerere na wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LE4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiagana na mjane wa Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere wakati walipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa, Msasani jijini Dar es salaam Januari 12, 2016 kuhani msiba wa Mbunge wa zamani, Leticia Nyerere. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
LE5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na Mjane wa baba wa taifa  Mama Maria Nyerere  (kushoto kwa Waziri Mkuu) baada ya kuhani msiba wa mbunge wa zamani, Leticia Nyerere,  Msasani jijini Dar es slaam Januari 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: