Kiongozi mkuu wa chuo
cha kiislam (Hawza) Imam Swadiq Maulana Sheikh HEMED JALALA amewataka
watanzania pamoja na viongozi wa Dini zote Duniani na wapenda Aman wote kuungana
kwa pamoja kulaani mauaji ya watu zaidi ya 40 akiwemo mwanazuoni mkubwa
Ayatollah Sheikh BAQIR NIMR yaliyotokea nchini Saudi Arabia tarehe 2,mwezi wa
kwanza mwaka huu.
Mauaji hayo ambayo
tayari yamedhibitishwa na wizara ya mambo ya ndani ya serikali ya Saudi Arabia
yanaelezwa kuwa yalitekelezwa kwa watu hao kuchinjwa hadharani baada ya
serikali Riyadhi kuwahukumu kifo kwa makosa ya kushiriki na kushawishi
maandamano.
Sheikh JALALA ambaye
pia ni mmoja ya viongozi wakuu wa kiroho wa waislam dhehebu la Shia Ithna
asherriya nchini Tanzania akizungumza na wanahabari kuhusu mauaji hayo ameeleza
kuwa wao kama watanzania wapenda amani na wapenda haki wameshikitishwa sana na
mauaji hayo ambayo amesema yanalenga kudidimiza haki za wanyonge ambazo
zilikuwa zinadaiwa na watu hao.
Mwanazuoni Ayatollah Sheikh BAQIR NIMR Enzi za uhai wake |
Amesema kuwa hukumu hiyo
ya kifo aliyohukumiwa mwanazuoni na mwanaharakati NIMR ni ya kikatili na msingi
wake ni kuivunja heshima ya binadamu ambaye hata katika vitabu vya dini mungu
ametaka aheshimiwe,huku akisema kuwa makosa yaliyotajwa na serikali hiyo juu ya
watu hao waliouawa hayakustahili adhabu hiyo kwani kumuua kiongozi mwenye
wafuasi kwa kosa la kudai haki za wanyonge ni kuamsha na kuchochea vurugu na
mizozo ya kidini ambayo imeanza kuibuka baada ya mauaji hayo ya kinyama.
Ayatollah Sheikh BAQIR NIMR picha ikionyesha moja ya siku ambazo alikuwa mikononi mwa polisi wa Saidi Arabia |
Baadhi ya mambo ambayo
mwanazuoni huyo Sheikh BAQIR NIMR pamoja na wenzake walikuwa wakiyapigania ni
pamoja na Uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wao kwa kura badala ya kuongozwa
kifalme,kutolewa na kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai
mabadiliko ya kiuongozi katika serikali,pamoja na kudai haki za binadamu
ziheshimiwe kwa kuwa kuna matabaka ndani ya nchi ambayo yanawanyima haki zao za
msingi.
No comments:
Post a Comment