Tuesday, January 12, 2016

FASTJET YAZINDUA SAFARI ZA NDEGE KATI YA DAR-NAIROBI NA DAR-ZANZIBAR.

mpu1
Mkurugenzi asiye mtendaji wa kampuni ya ndege ya Fastjet Balozi Ami Mpungwe, akizungumza na wasafiri wakati wa kuanzisha safari za ndege hiyo kwenda Nairobi kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni mkurugenzi asiye mtendaji Lawrence Masha, Meneja mkuu wa kampuni hiyo (Afrika Mashariki) Jimmy Kibati na Meneja wa mahusiano kati ya Fastjet na Serikali, Mhandisi August Kowero.
mpu2
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, John Haule (kulia) akikata utepe ili kuikaribisha ndege ya Fastjet nchini Jijini Nairobi mara baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jana, kushoto kwake ni Meneja mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki Jimmy Kibati na Mkurugenzi asiye mtendaji balozi Ami Mpungwe.
mpu4
Wageni mashuhuri wakishirikiana na viongozi wa Fastjet kukata keki mara baada ya ndege kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jana, kutoka kushoto ni Meneja mkuu  wa Fastjet Afrika Mashariki Jimmy Kibati, mkurugenzi asiye mtendaji Ami Mpungwe, Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule, Mkurugenzi asiye mtendaji Lawrence Masha na Meneja Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini Kenya (KAA) William Simbah.
mpu5
Ndege ya Shirika la Ndege la fastjet ilikiwasili kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwa mara ya kwanza baada ya kuanza safari zake kati ya Dar es Salaam na Nairobi nchini Kenya
mpu6
Meneja mkuu wa kampuni hiyo (Afrika Mashariki) Jimmy Kibati juu pamoja na wafanyakazi wa Ndege hiyo wakishuka kwenye ndege mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.
mpu7
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, John Haule (kulia) akiwa katikapicha ya pamoja na Meneja mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki Jimmy Kibati na Mkurugenzi asiye mtendaji balozi Ami Mpungwe mara baada ya  kuikaribisha ndege ya Fastjet nchini Jijini Nairobi wakati  ndege hiyo kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jana, kwa mara ya kwanza.

……………………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya ndege ya Kiafrika yenye gharama nafuu fastjet,imepanua mtandao wake  wa safari barani Afrika kwa kuwa na safari za kimataifa za kila siku  kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro kwenda Nairobi na hali kadhalika  safari za ndani  za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Uzinduzi wa safari za anga za fastjet  kutoka Dar es Salaam hadi Nairobi, Kilimanjaro hadi Nairobi na Dar e s Salaam kwenda Zanzibar zote zimefanyika Januari 11, 2016 na hivyo kufanya iwe ni hatua muhimu katika kujipanua katika safari zake kimataifa na kitaifa.
Safari za kila siku kwenda Zanzibar  zinatarajiwa kuwarahisishia watanzania walio wengi pamoja na wageni wa kimataifa kuitembelea Zanzibar,kukuza utalii na biashara  pamoja na kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye kukua kwa uchumi visiwani humo.
 Kuzinduliwa kwa safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam kunaanzisha enzi mpya  ya abiria ambao wamekuwa wakitaabika kwa tozo kubwa ya nauli kwa usafiri wa anga  kati ya nchi mbili za Afrika Mashariki  ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.
Matokeo ya safari za fastjet nchini Kenya tayari yameshaanza kujadiliwa, yakikolezwa na ukweli kwamba nauli dhidi ya mashirika washindani  yanayofanya safari kati ya nchi hizi mbili ambako ni kushuka kwa kasi hadi ya asilimia 40  siku ya kwanza tu tangu fastjet
ilipotangaza  kuanzishwakwa safari zake  kati ya Kenya  na Tanzania.
Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse anasema, “ukweli ni kwamba ushindani ni mzuri kwa abiria. Unaleta nafasi kuchagua jinsi ya kusafiri na pia unasababisha nauli kushuka.”
Nauli za fastjet kimsingi ziko chini  kuliko nauli zinazotozwa na mashirika mengineya ndege  ambayo hivi sasa yanafanya safari kati ya Tanzania na Kenya ambapo nauli za fastjet kutoka
Kilimanjaro/Nairobi ni kuanzia dola 50 kw safari  moja na ya kwenda Dar es Salaam/Nairobi
ni dola 80 kwa safari moja. Nauli hizo hazijumuishi kodi za serikali ambazo ni dola
49kwa kuondokea Tanzania na dola 40 kwa kuondokea Kenya na hivyo  fastjet
kuwashauri abiria  kukata tiketi zao mapema  ili kuitumia fursa hiyo ya nauli ya bei
nafuu. fastjet inatarajia kuongeza safari moja zaidi kwenye niia yake mpya ya Kenya
 kutokan ana mahitaji ya wateja kuongezeka kutokana na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati na tayari imeshaonesha kwamba inatarajia kuzindua safari kati ya
Zanzibar na Nairobi na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka huu 2016.
“Kama ambavyo imekuwa kwa njia zetu nyingine ambazo fastjen timezindua tunatarajia  abiria wetu walio wengi kwenye njia yetu mpya Kenya kuwa abiria wa kwanza  ambao huenda  wasingemudu kusafiri kwa  njia ya anga hapo awali,” anabainisha Corse.
 Matarajio haya yanaungwa mkono na utafiti  uliofanywa na fastjet ambao unaonesha
Kuwa zaidi ya theluthi moja ya abiria watakuwa wanasafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza na hali kadhalika kumudu usafiri huo kwa mara ya kwanza.
 “Usafiri wa anga ambao abiria wanaumudu  ni msingi wa kukua kwa uchumi  barani Afrika kutokana na matokeo chanya yanayosababishwa na bei nafuu ya usafiri wa ndege kwa maisha ya wananchi na uchumi kwa jumla,”alisema Corse.
“Tunazishukuru wizara za usafirishaji na mamlaka za usafiri wa anga za Tanzania na Kenya  kwa kufanya kazi pamoja  kuwezesha fastjet kutambua dira yetu ya kuongezeka kwa idadi ya wateja  ambao wanaweza kufikia usafiri wa anga wanaoumudu,” alihitimisha Corse.
 Jambo ambalo lina umuhimu zaidi kwenye njia hii mpya ni njia mbadala ya kuibeba mizigo inayojulikana kama “freighty” ambayo inaruhusu abiria  kusafiri na mzigo  hadi kilo 80 kwenye mabegi kwa dola 80. Mbadala huu wa mzigo kimsingi unatarajiwa kuwa maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet kununua bidhaa za jumla na kuzisafirisha kwa ajili ya kuuzakwenye masoko ya ndani.  Ukataji tiketi unaweza kufanyika  kupitia mtandao wa www.fastjet.com, kupitia wakala waliothibitishwa na fastjet au kwa njia ya mawasiliano ya simu: +255-784-108900.  Malipo ya tiketi yanaweza kufanyika kwa fedha taslim, kwa njia ya mtandao au kupitia malipo kwa njia ya simu.

No comments: