Tuesday, January 5, 2016

Zaidi Ya nyumba 100 zaezuliwa kwa upepo mkali huko Tandahimba,soma hii


Pichani ni mbunge Jimbo la Tandahimba mkoani mtwara Katani Ahamed aliyetangulia hivi karibuni akiwatembelea wahanga katika kata ya Chaume  jimboni humo kufuatia upepo mkali uliyoambatana na mvua kunyesha anayefata ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chaume Tauka Yusufu wengine ni wanafunzi wakisadia kuokota bati zilizoezuliwa
Haika Kimaro Tandahimba



ZAIDI ya nyumba 100 zimeezuliwa na nyingine kubomoka kufuatia upepo mkali uliyoambatana na mvua kunyesha hivi karibuni katika Kata ya Chaume halmashauri ya Tandahimba mkoani mtwara. 


Upepo huo uliyodumu kwa takribani dakika tatu umesabisha maafa makubwa kwenye kata hiyo katika vijiji viwili ikiwemo  Chaume na Sokoine  na kusababisha familia zikikosa mahali pa kuishi huku zikipata hifadhi toka kwa jirani zao ambao kunusurika na janga hilo.


Aidha, tukio hilo limewagusa viongozi mbalimbali katika halmashuri hiyo na mkoa kwa jumla ambapo mbunge wa Jimbo hilo la Tandahimba Katani Ahmedi  baada ya kuwatembelea wahanga hao na  kuwapa faraja alisema kuwa,  wao kama halmashauri watafanya kila jitihada ya kuwasaidia wale wote waliyokubwa na janga hilo.

“Niwaombe tu ndugu wananchi kufuatia tukio hili naomba tuwe na subira katika kipindi hiki kwani hili jambo ni letu sote hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu huku tukimshukuru mwenyezi mungu kwa kile kilichotokea huku tukisubiri taratibu zingine ziendelee”,Alisema Katani


Pichani ni mbunge Jimbo la Tandahimba mkoani mtwara Katani Ahamed hivi karibuni akitoa majumuisho ya ziara yake baada ya kuwatembelea wahanga katika kata ya Chaume  jimboni humo kufuatia upepo mkali uliyoambatana na mvua kunyesha anayefata ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chaume Tauka Yusufu wengine ni wanafunzi wakisadia kuokota bati zilizoezuliwa.
Hata hivyo alisema kuwa, jambo hilo mbali tu na nyumba kubomolewa bali hata shule imeweza kuezuliwa hali ambayo inawalazimu kuhakikisha jitihada za kusimamia zoezi la ujenzi huo unafanyika kwa haraka kutokana shule zinatarijia kufunguliwa hivi karibuni. 

Pia mwenyekiti wa halmashauri hiyo Namkulya Sulemani alisema,  wao kama viongozi na jamii kwa jumla kwa kiasi kikubwa wameguswa na jambo hilo ila kikubwa cha kushukuru halikuweza kuleta madhara makubwa ikilinganishwa na ukubwa wa tukio hilo.

Alisema, wao kama serikali wanatambua athari waliyoipata wakazi hao kwani jambo hilo limewagusa wadau wengi hivyo wavumilivu kutokana jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha mambo yanakaa sawa hivyo wako pamoja nao katika kipindi hicho kigumu.

Salma Hatibu mkazi wa kijiji hicho cha Sokoine huku akizungumza kwa masikitiko kuhusiana na janga hilo alisema, upepo na mvua hiyo umewasababisha hasara kubwa kwani  mapaa ya nyumba zao mbili zimezuliwa, mikorosho imeanguka na kuharibifu wa vyakula vilivyoifadhiwa ndani hivyo anaomba msaada kwa yeyote atakayeguswa na jambo hilo ikiwemo  makampuni na watu binafsi.

Naye Hassan Mzee mkazi wa Chaume alisema kuwa, wao kama wakazi wa kata hiyo tukio hilo wameshukuru msada huo uliyotolewa na mjumbe huyo kwan msada huo ni mkubwa sana kwao na jambo hilo  limewarudisha nyuma kimaendeleo kwa kuwa ni kipindi kigumu kwao kutokana hawana mahali pa kuishi wala chakua na hawajuwi wataanzia wapi kurudi katika hali zao za kawaida kimaisha na bado mvua zinaendelea kunyesha  hivyo kuitaka serikali kuharakisha jambo hilo. 

No comments: