Mbunge wa Temeke mh.ABDALA MTOLEA akiwa katika ziara katika Jimbo lake leo kutizama changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake |
Mbunge wa Temeke mh.ABDALA MTOLEA,amefanya ziara katika jimbo
lake ili kujua changamoto zinazo wakabili wananchi wajimbo hilo.Akizungumza hii
leo MH.MTOREA, na wanachi katika kata ya CHANG'OMBE,Huku wananchi wakitoa kero
zao mbalimbali.
Swala kubwa likiwemo uvaminzi wamaeneo ya wazikiwemo watu kuvamia maeneo hayo na kuyafanya makazi,wengine kuchukua na kuweka
viwanda,tatizo la huduma mbovu ya afya,na uchafu katika mifereji ya maji
machafu,mh.MTOREA,amesema atashugurikia kero hizo atajitahid kwa uwezo wake
wote kutatua kero hizo kwa wakati huku ukizingatia sasa serikali ni sikivu
hivyo amewataka wananchi hao kuwa na subira.
Akizungumza mmoja wa wananchi wa kata hiyo ya
changombe,HARIMA MATOGORO amesema wanapata shida sana kwa kuvamiwa maeneo mengi
ya wazi katika kata hiyo ikiwemo eneo
lililopo tololi changombe kuuzwa na mmiliki wa eneo hilo kuweka kiwanda cha
fenicha ambaye mmiliki wake ni OIL COM ,ambacho hutiririsha maji machafu nje ya
makazi ya watu.
Pia hakuishia hapo amelalamikia huduma ya afya katika
zahanati ya kata hiyo kuwa ni mbaya,ikiwemo miundo mbinu ya kutorizisha
,vilevile ukosefu wa dawa,na wauguzi kuchelewa kuingia ofisini ambapo wanaingia saa
tatu na kutoka saa nane,ivyo amemtaka mbunge kufanyia kazi kero zao
hizo
Pia mtolea amewataka wananchi kushirikiana nae bila kujal
itikadi za vyama vyao vilevile amewataka wananchi kuchukia uchafu kutoka moyoni
kwan ndicho chanzo cha magonjwa mbalimbali ya mlipuko,ikiwemo
kipindupindu,ivyokuwataka wasafishe mazingira yao kuwa safi wakat wote
Baadhi ya changamoto ya mitaro ya maji machafu aliyojionea mbunge huyo |
Aidha,diwani wa kata hiyo mh.BENARD NDALUCHAKO
amewataka wananchi kubadilika na kutoa ushirikiano kwa viongozi, ikiwemo
kuhuzuria katika vikao vya kata na mtaa bila kujali itikadi za vyama kwani bila
wananchi kuonesha ushirikiano kwao hawawezi kufika mbali na
kutekeleza ahadi hizo kwa usahii ivyo,ushirikiano wa wananchi ni
muhimu kwao
No comments:
Post a Comment