Thursday, February 4, 2016

KINANA ASHIRIKI KAZI ZA MIKONO MKOANI SINGIDA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida ambapo alipokea taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM pamoja na kushiriki kupaka rangi ofisi za CCM mkoa wa Singida.
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku (kushoto)akisoma taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM  kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupokea taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na kamati ya
siasa ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupokea taarifa za maandalizi
ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la  CCM mkoa wa Singida ikiwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Mwalimu Mussa Ramadhan Sima akishiriki kupaka rangi pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jengo la ofisi za CCM mkoa wa Singida ikiwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo

No comments: