Wednesday, February 3, 2016

USISHANGAE---TIGO SASA HUDUMA YA WATSAPP NI BUREEEEE KABISA.FURAHIA



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mikononi Tigo,
Diego Gutierrez, akizungumzia uzinduzi huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam usiku wa Februari 2, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


KAMPUNI ya simu za mikononi Tigo, imezindua huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wake kuanzia Usiku wa Februari 2, 2016, wateja watakuwa wanachat bure. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, 

 Diego Gutierrez amewaambia wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam
“Ushirikiano huu ni wakwanza nawaina yake katika sekta ya mawasiliano hapanchini.” Aliandika Diego kwenye WhatsApp yale iliyorushwa moja kwa moja kupitia screen kubwa iliyokuwa ukumbini.

“Ushirikiano huu wa kihistoria una maa kuwa, wateja wa Tigo sasa ni sehemu ya familia kubwa ya kimataifa ya watumiaji Milioni 900 na huduma ya WhatsApp Duniani.” Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Tigo.

“Na hii ni namna yetu ya kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu kwa kuwapa huduma bora na za viwango vya juu zaidi kwa lengo la kuwafurahisha wateja wetu wa tigo.” Alimaliza ujumbe wake Mkurugenzi huyo wa tigo.
Tigo ambayo kwa sasa ina jumla ya wateja Milioni 10 waliosajiliwa na kutoa ajira 300,000 kote nchini ilianzishwa mnamo mwaka 1994.


 Ujumbe wa Mkurugenzi Mtendajiwa Tigo
 Ilikuwa ni furaha na usiku wa mask


 wakichukua Selfie tayari kWhatsaap jamaa na marafiki bureeee








 Wageni waalikwa wakifuatilia
  Diego Gutierrez, akiandika ujumbe wa uzinduzi wa Whatsaap ya bure
 Diego Gutierrez, akizungumza jambo na msanii maarufu wa vichekesho hapa nchini, JOTI, (katikati) na meneja wake Betty Nelson
 Diego akiwashukuru washereheshaji
Diaego akitoa hotuba
HABARI KWA MSAADA WA http://khalfansaid.blogspot.com/

No comments: