Wednesday, February 3, 2016

Wanachama wa mifuko ya hifadhi za kijamii watakiwa kutunza kumbukumbu zao

Katikati ni mkuu wa wilaya ya mtwara FATUMA ALLY,kulia ni meneja wa PPF kanda ya kusini KWAME TEMU,kushoto aliyevaa black ni meneja masoko ELIHURUMA NGOWO wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa toka Taasisi mbalimbali mkoani mtwara juu ya kazi zinazofanywa na mfuko wa Pension wa PPF
Haika Kimaro


Mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kushirikiana na wananchamana wametakiwa kuhifadhi kumbukumbu za makato yao ya kuchangia mifuko yao ili kuondoa usumbufu wakati wa uchukuaji mafao wakati wanapostaafu.


Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara,Fatuma Ally wakati wa ufunguzi wa semina iilyoandaliwa na mfuko wa pensheni wa PPF liyohusisha maafisa toka taasisi mbalimbali mkoani Mtwara juu ya kazi zinazofanywa na mfuko huo.

Alisema kuwa mara kwa mara viongozi wamekuwa wakipokea malalamiko yanayohusiana na ukatwaji wa pesa kwaajili ya kuchangia mifuko hasa pale muda wa kustaafu unapofika.

" Mifuko yote ya hifadhi ya jamii ijitahidi kuhifadhi kumbukumbu za waajiri wao ili kila mmoja ajitambue na mhusika aandae nyaraka zake ili pindi anapoenda kuchukua mafao yake baada ya kustaafu asianze kusumbuliwa kwani malalamiko yote tunayopokea baada ya mtu kustaafu  unaambiwa kumbukumbu za mlengwa hazikuwa sawa,"alisema Ally
Aidha alisema kuna wakati michango ya waajiriwa imekuwa haipelekwi na mwisho mhusika anajikuta anakatwa pasipo kupata stahiki zao huku baadhi wakikatwa kiasi kikubwa lakini kinachopelekwa ni kidogo.

Hata hivyo alisema serikali inatambua mifuko ya hifadhi ya jamii inawafikia watu wachache licha ya kuwa na uhitaji mkubwa na kuitaka mifuko hiyo kutembelea wahusika maofisini na kuwashawishi badala ya kuwaamuru.
Akizungumza meneja wa mfuko wa PPF kanda ya kusini,Kwame Temu alisema mfuko huo umeanzisha sehemu mpya inayoitwa 'Wote scheme',mpango utakaosaidia watu wote hata wenye kipato kidogo kuweza kujiunga na PPF .
Alisema kila mwanachama ataweza kuchangia Sh 20,000 na kuendelea kwa mwezi.

" Sasa hivi mfuko wa PPF imeanzisha sehemu mpya inayoitwa 'wote scheme' na mpango huu utasaidia watu wote hata wenye kipato kidogo kuweza kujiunga na PPF na kadri siku zinavyoenda mfuko umekuwa ukibuni mbinu mpya ili kuwafikia wananchi wengi kwa zaidi,"alisema Temu

No comments: