Thursday, March 31, 2016

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 1,2016 YAPO HAPA

SPIKA WA BUNGE AKUATANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA AHMADIYYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA

jam01
. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana  na Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Sheik Tahir Mahmoud aliyemtembelea pamoja na viongozi wenzake Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
jam2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kiongozi wa Jumuiya hiyo nchini Sheik Tahir Mahmoud.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (BARA) AWATAKA WATUMISHI WA CCM KWENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA SASA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, akiwa katika ziara ya kikazi leo. Anayemsalimia ni Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali Abdallah Mpokwa.  Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo Mwangi Kundya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia ni Katibu ambaye hajapangiwa kituo, Mariam Yusuf

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA

mpanjuMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Ndugu Amon Mpanju wakati Naibu Mpanjo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo March 31, 2016.(Picha na OMR)

Wednesday, March 30, 2016

IZZO BIZNESS APAGAWISHA WAKAZI WA MBEYA KWENYE TAMASHA LA PASAKA

Msanii Emmanuel Simwinga maarufu “ Izzo Bizness “ akitumbuiza
kwenye tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya
jumapili iliyopita.
 Izzo Bizness  akishow love kwa mashabiki zake tamasha la pasaka la home Sweet Home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya
jumapili iliyopita
Mamia ya mashabiki wakifurahia burudani toka kwa Izzo  Bizness
Yani ilikuwa shangwe wakati Izzo Bizness akitumbuiza jukwaani kwenye  tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya jumapili iliyopita

Tuesday, March 29, 2016

MSANII KLEYAH AWAPAGAWISHA MASHABIKI VIWANJA VYA ESCAPE ONE MKESHA WA PASAKA


Msanii wa usic wa kizazi kipya nchini Tanzania anayekuja kwa kasi kwa sasa KLEYAH mwishoni mwa wiki hii aliwapagawisha mashabiki wake wa Jiji la Dar es salaam katika viwanja vya ESCAPE ONE kwa kutoa burudani kali ya kutambulisha wimbo wake mpya wa AFRICAN DRUM ambao unamuweka juu kwa sasa katika anga za music wa kitanzania. 


 Katika tamasha hilo ambalo liliandaliwa na Clouds FM lililowakutanisha wasanii maarufu nchini akiwemo Dogo Janja,Godzila,Q CHIEF,MB DOG na wengine wengi Msanii KLEYAH Alipata nafasi ya kutambulisha nyimbo yake mpya na kupokelewa kwa sangwe kubwa kutoka kwa watanzania waliohudhuria Tamasha hilo lililofanyika Usiku wa mkesha wa pasaka.
 Akizngumza baada ya kufanya shoo yake msanii huyo aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano na mapokezi makubwa aliyoyapata na kuahidi kuendelea kutoa burudani na kuhakikiaha kuwa anawsaburudisha watanzania kwa kupitia kipaji chake.
Hapa kuna picha zote za tukio hilo unaweza kuzitazama

Mbowe na Watanzania Zaidi Ya 600 Wafanya Tukio Kubwa Kwa Lowassa

http://www.jamiiforums.com/attachments/img-20160328-wa0120-jpg.333118/FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa; na kwamba matokeo hayo yawe chachu ya kufanya vizuri zaidi katika uchaguzi ujao, anaandika Josephat Isango.

Alisema uchaguzi si tukio, bali mchakato; na kwamba kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasa ya urais, watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi na matokeo yake. Alisema matokeo hayo yanapswa kuwatia hasira na kuwahamasisha waendelee kupambana,

http://www.jamiiforums.com/attachments/img-20160328-wa0121-jpg.333121/Mbowe amesema hayo Masaki, nyumbani kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajili yake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,” alisema Mbowe.

Aliongeza kwamba, kazi ya mapambano wanayofanya viongozi sasa ina manufaa kwa kizazi kijacho, na kama wanaoifanya sasa wakafanikiwa kuonja matunda ya kazi ya mikono yao basi ni jambo la kumshukuru Mungu.

“Kazi anayofanya Lowassa (Baba Kadeti) si lazima aone matunda yake leo, huenda mtoto wake ataonja na asipoonja Kadeti basi wajukuu wataonja matunda hayo na kutambua mchango mzuri wa babu yao kwa kazi kubwa ya maana anayofanya sasa,” alisema.

http://www.jamiiforums.com/attachments/img-20160328-wa0117-jpg.333120/Aliwahimiza Watanzania zaidi ya 600 waliokuwepo kwenye halfa hiyo kuwa wale walio wafuasi wa vyama vya siasa hata wasio na vyama wana wajibu wa kuendelea kwa nguvu zote na kazi ya kupambana ambayo Lowassa amejiunga nayo, kwani wakati wa uchaguzi watu wengi walipigana kumsaidia sio kwa ajili ya familia yake ila walifanya vile kwa sababu ya nchi hii huku Lowassa akiwa kiongozi na mpeperusha bendera.

Mbowe alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania waendelee kumwombea neema, ujasiri na afya njema Lowassa kwani taifa bado linamhitaji kuliko pengine anavyohitajika na familia yake.

Aidha, Mbowe alimsifu pia Regina, mke wa Lowassa, kwa ujasiri wake na familia nzima kwa uamuzi mzuri na ujasiri aliochukua katika kuhakikisha Watanzania wanatafuta haki na ujasiri kwa kukata minyororo ya watesi.

“Mama ulikuwa jasiri kwenye kampeni katikahatrua za awali, lakini baadaye ulipata ujasiri zaidi kama mgombea wetu wa urais (Lowassa) lakini baadaye ulipata ujasiri zaidi hata kuliko wanasiasa wengine, asante sana kwa kuondoa woga, asante kwa kuongoza familia na wote tuendelee na mapambano.” alihimiza Mbowe.

http://www.jamiiforums.com/attachments/img-20160328-wa0116-jpg.333119/Kabla ya Mbowe kusimama, neno la kuwashukuru watu waliofika nyumbani lilitolewa na Regina akasema familia, hasa Lowassa mwenyewe, ilikuwa inasubiri kwa hamu siku ya kumshuruku Mungu na Watanzania kwa mazuri mengi aliyowatendea.

Hafla hiyo ya shukrani ilianzia kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Dar es Salaam. Lilichagizwa na nyimbo kadhaa za shukrani zilizopendkeza na Lowassa mwenyewe, na kuimbwa na washiriki wote, wakiwamo wa madhehebu mengine ya dini.

Miongoni mwa washiriki wa hafla hiyo ni baadhi ya wanachama wapya wa UKAWA waliojiengua CCM mwaka jana, wakiwamo Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Lawrence Masha, John Guninita, na wengine.

Ilihudhuriwa pia na wanasiasa, viongozi wa dini wa madhehembu mbalimbali, vijana na wazee, matajiri na watu wa kawaida kutoka sehemu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.

“Tumepata mengi mazuri, tunaweza kusafiri kwenda Monduli na kurudi si sababu tuna magari mazuri kuliko wengine; tunaweza kusafiri kwa ndege na tukarudi salama, lakin hata wakati mwingine unasikia mtu anakupigia simu kukusalimu au kukuandikia ujumbe mzuri wa faraja, haya yote ni sababu ya Mungu na tukaona leo tufike Kanisani kusema Mungu asante kwa mema yote uliyotujalia,” alisema Regina akiwa amejawa tabasamu muda wote, huku akishangiliwa.

http://www.jamiiforums.com/attachments/e9826da8-88a5-40d3-af99-74345d651834-620x312-jpeg.333116/Wajukuu wa Lowassa walijumuika kumwimbia babu yao wimbo kutoka miongoni mwa tenzi za Injili zilizoandaliwa kwa ajili hiyo, huku wakiongozwa na mpiga kinanda.

Baada ya wajukuu, Masha alitumbuiza washiriki kwa wimbo wa Kiingereza “Amazing Grace,” akatuzwa kiasi cha Tsh. 50,000 ambacho, hata hivyo, alikigawa kwa wajukuu wa Lowassa.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Lowassa aligombea urais mwenye mvuto kuliko wote, lakini aliibuka mshindi wa pili katika matokeo yenye utata, akiwa nyuma ya John Magufuli.  

TIGO YATOA 300M/- KUDHAMINI WANAFUNZI WA TEHAMA VYUO VIKUU

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael.
 
Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katikati ni Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez,na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael. wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.
 
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  akipeana mkono na Mmoja wa wanafunzi waliopata udhamini wa tigo  Carolyne Paul, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Udsm shahada ya uhandisi wa kompyuta na teknolojia ya habari   wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati),Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula(kulia) na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael(kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati) akipata “SELFIE”  na ,Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula  na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam   .

SERIKALI YA TANZANIA KUJENGA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA TANGA HADI UGANDA.

1Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
2Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Sekta ya Mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Ally Daud- Maelezo

Friday, March 25, 2016

MSTAHIKI meya wa halmashauri ya Temeke Abdalah Chaurembo amelitaka balaza la madiwani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao


                                                                                                                     MSTAHIKI meya wa halmashauri ya Temeke Abdalah Chaurembo amelitaka balaza la madiwani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao ili kuboresha na kukuza mapato yao ya ndani  kwaajili ya kuweza kufikia malengo yao ya kutekeleza shughuli za maendeleo ya jamii.

Hayo aliyasema jana  na mstahiki meya huyo wakati wa balaza la madiwani katika kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017.

Akizungumza na madiwani wa balaza hilo Mstahiki meya wa Temeke,alisema kuwa madiwani wanatakiwa kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa kuwabana watendaji wao ili  kuongeza jitihada katika kuhakikisha halmashauri yake inapata fedha za kutosha za kuboresha shughuli mbali mbali za kijamii katika kipindi cha mwaka wa
fedha wa 2016/2017.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo alisema kuwa makadirio ya mapato ya  Halmashauri yake kwa mwaka 2016/2017 ni
sh bil 231,685,350,340.00 ambapo sh bil 50,285,639,000.00  ni sawa na asilimia 21 ni  mapato kutoka vyanzo vyandani,ruzuku kutoka serikali kuu na mishahara nibil 105,151,112,288.00,fedha za maendeleo ni bil 18,542,688,852,00,Bil 57,069,696,000.00 miradi ya DMDP,na wafadhili ni sh  mil 636,204,200.00.

Alisema kuwa Halmashauri yake imejipanga kuongeza nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa kodi ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipakodi kwakuwa shughuli za maendeleo ya nchi yanatokana na kodi hivyo ni muhimu kila jamii kutambua umuhimu wa kulipa kodi ili kuchochea kuongezeka kwa shughuli za maendeleo
ya taifa letu.
Naye Diwani wa kata ya mbagala kuu Yusuph Manji amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutafuta namna na njia mbadala za kuhakikisha Manispaa ya Temeke inakuwa na mifumo mizuri itakayoiwezesha kujitegemea katika kusimamia shughuli za maendeleo ya ndani bila kuwa tegemezi kwa wafadhili na serikali kuu.

"kwa mujibu wa tamko la mkuu wa mkoa kwamba halmashauri zinatakiwa kujitegemea zenyewe ili kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu,na wafadhili hivyo lazima kuboresha ukusanyaji wa mapato
ya ndani"alisema.