
Hayo aliyasema jana na mstahiki meya huyo wakati wa balaza la madiwani katika kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017.
Akizungumza na madiwani wa balaza hilo Mstahiki meya wa Temeke,alisema kuwa madiwani wanatakiwa kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa kuwabana watendaji wao ili kuongeza jitihada katika kuhakikisha halmashauri yake inapata fedha za kutosha za kuboresha shughuli mbali mbali za kijamii katika kipindi cha mwaka wa
fedha wa 2016/2017.

sh bil 231,685,350,340.00 ambapo sh bil 50,285,639,000.00 ni sawa na asilimia 21 ni mapato kutoka vyanzo vyandani,ruzuku kutoka serikali kuu na mishahara nibil 105,151,112,288.00,fedha za maendeleo ni bil 18,542,688,852,00,Bil 57,069,696,000.00 miradi ya DMDP,na wafadhili ni sh mil 636,204,200.00.
Alisema kuwa Halmashauri yake imejipanga kuongeza nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa kodi ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipakodi kwakuwa shughuli za maendeleo ya nchi yanatokana na kodi hivyo ni muhimu kila jamii kutambua umuhimu wa kulipa kodi ili kuchochea kuongezeka kwa shughuli za maendeleo
ya taifa letu.

"kwa mujibu wa tamko la mkuu wa mkoa kwamba halmashauri zinatakiwa kujitegemea zenyewe ili kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu,na wafadhili hivyo lazima kuboresha ukusanyaji wa mapato
ya ndani"alisema.
No comments:
Post a Comment