Friday, March 18, 2016

Mbunge wa Ndanda Chadema Cecil Mwambe apingwa mahakamani,kesi ya uchaguzi yaanza kusikilizwa

Mahakama Kuu kanda Mtwara Wilaya ya Masasi imeanza Kusikiliza Kesi ya Uchaguzi no 3 ya mwaka 2015 inayomkabili Mbunge wa Ndanda kupitia Chadema Cecil Mwambe iliyofunguliwa na Aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Ccm Mariam Kasembe kwa Tuhuma za kutoa Lugha ya kuudhi kipindi cha Uchaguzi.     Mahakama hiyo imemtaka mshtaka kuleta Mashahidi 80 Tayar kwa Kuanzia kusikiliza kesi hiyo April 20 Mwaka Huu.


Kesi Hiyo Ambayo imehamishwa kutoka Mtwara na kuletwa katika office za mahakama ya Wilaya ilianza kusikilizwa Asubuh kwa mawakili wa pande zote mbili kukubaliana Mashataka ambayo yataelenga kupata Mashahidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji wa mahakama Kuu ya Dar es salaam Winfrida Korosso ambaye amewataka upande wa mashtaka kuhakikisha tareh20 April kesi inaanza kusikilizwa kwa Mashahidi 80 kutoa Ushahidi.

Mwanasheria aanemtetea Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe Tundu Lissu amesema tayari kesi inaonekana kufika sehem inayopaswa ili haki iweze kutendeka.
"Tumemaliza maandalizi yote ya awali kilichobaki tunaingia kwenye mpambano wenyewe kuna Maeneo 10 yanayohitaji kujadiliwa siwezi kuyataja moja baada ya jimhine lakini tuhuma zote za msingi ambazo zimetolewa na mlalamikaji na ambayo zimekataliwa nawajibu 
maombi,"alisema Lissu

Kwa upande wa mawakili wa upande wa Mshataka kugoma kuongea na waandishi kwa madai kuwa kesi iliyopita alihojiwa lakini hakuona Katika chombo chochote cha Habar."Hatutak kuongea na waandishi wa Habar mbona mlituhoji na hatukuona Popote.Alisema mmoja wa mawakili wa Mariam Kasembe.

No comments: