Friday, March 18, 2016

TWIGA STARS KUWAFUATA ZIMBABWE LEO


Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu “Twiga Stars” unatarajiwa kuondoka leo majira ya saa 4 usiku kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake utakaochezwa siku ya Jumapili mjini Harare.

Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu, Nasra Juma inaondoka ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano, baaada ya kuwa kambini kwa takribani wiki mbili kwa maandalizi ya mchezo huo.

Nasra amesema makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita nyumbani, wameyafanyia kazi na sasa wana imani ya kufanya vizuri siku ya Jumapili katika uwanja wa Rufaro mjini Harare na kuweza kusonga mbele katika hatua ya pili.
Mkuu wa msafara ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake TFF, Amina Karuma, benchi la ufundi litaongozwa na kocha mkuu Nasra Juma, kocha msaidizie Elyutery Muholery, kocha msaidizi Edina Lema, daktari wa timu Anange Lwila, mtunza vifaa Esther Chaburuma na meneja wa timu Furaha Francis.
Wachezaji wanaosafiri leo ni Fatuma Omary, Stumai Abdallah, Maimuna Khamis, Fatuma Issa, Anastazia Katunzi, Donisia Minja, Happyness Mwaipaja, Wema Richard na Amina Bilal.
Wengine ni Asha Rashid, Mwanahamis Omary, Belina Julius, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatibu, Mwajuma Abdallah, Amina Ramadhani, Fatuma Mustafapha na Neema Kiniga.

No comments: