Friday, March 18, 2016

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILANO AKABIDHI BAISKELI KWA WALEMAVU

Naibu waziri Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akikabidhi baskeli 10 kwa baadhi ya watu wenye mahitaji maalumu ya viungo mkoani Mtwara.Katikati ni Msajili wa Bodi,mbunifu Majengo,Jehad Jehad.Amekabidhi baskeli hizo wakati wa semina endelevu ya 25 ya Bodi ua Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi mkoani Mtwara.

.Naibu waziri Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akikabidhi baskeli 10 kwa baadhi ya watu wenye mahitaji maalumu ya viungo mkoani Mtwara.Kulia ni Msajili wa Bodi,mbunifu Majengo,Jehad Jehad,Mwenyekiti wa Bodi,Dk Tonnie Mwakyusa akifuatiwa na katibu wa watu wenye mahitaji maalumu mkoani Mtwara, Abdallah Chiwahula.Amekabidhi baskeli hizo wakati wa semina endelevu ya 25 ya Bodi ua Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi mkoani Mtwara.


Mtwara.Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amewataka wataalamu wa ujenzi nchini kutekelea majukumu yao kwa uadilifu na weledi ili kuleta manufaa kwa kwa jamii na kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayanasi na teknolojia.

Ngonyani ameyasema hayo mkoani Mtwara kwa niaba ya waziri Makame wakati wa ufunguzi wa semina endelevu ya 25 ya bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi iliyofanyika mkoani hapa na kubainisha kuwa sekta hiyo imekuwa na heshima kubwa tangu kuanzishwa.

Amesema kuwa sekta hiyo imekuwa na  mchango mkubwa nchini na imekua ikiwategemea kwa kiasi kikubwa wataalamu hao hivyo ni furaha yake kuhakikisha utendaji kazi wao unakua wa weledi na manufaa kwa jamii katika Nyanja zote.

“Unajua Mtwara ya sasa siyo kama ya zamani kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika sekta ya ujenzi kasi yake huwezi kuifananisha na miaka ya nyuma sasa furaha yangu ni kuona wataalamu wanafanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubora unaotakiwa,”alisema Mhandisi Ngonyaji na kuongeza

 “Nimesikia moja wapo wa malengo ya semina hizi ni kuwawezesha wataalamu wa fani hii kwenda na wakati kwa maana kujiongoezea ujuzi wa kitaalamu ili kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia na kuwawezesha wataalamu kutenga majukumu yao kwa weledi licha ya kuwa kuna baadhi ya changamoto,”aliongeza Mhandisi Ngonyani

Akizungumza mwenyekiti wa bodi hiyo Mhandisi Dk Tonnie Mwakyusa alisema kuwa katika utendaji kazi wa wataalamu wao bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiewemo uelewa mdogo kwa baadhi ya waendelezaji kuhusiana na suala zima la umuhimu wa kutumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika kubuni na kutekeleza miradi yao.

Amesema kuwa bodi hiyo imekuwa ikihimiza wadau na waendelezaji wote wa miradi kuhakikisha kila mradi wa matumizi ya umma na ile ya binafsi inayozidi thamani ya Sh 150 mil kuwatumia wabunifu wa majengo na wakadiriaji majenzi katika kubuni na kusimamia miradi ikiwa ni kutekeleza matakwa ya sheria Na. 4 ya mwaka 2010.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali kupitia wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano kwa kutuunga mkono katika masuala mbalimbali ya kisera na kifedha licha ya kuwa kuna baadhi ya waendelezaji kuhusiana na suala nzima la umuhimu a kutumia wabunifu na kusimamia miradi kwa kutekeleza matakwa ya shera namba 4 ya mwaka 2010,”alisema Dk Mwakyusa 


Alisema wataalamu hao wanahitaji kutambua mahitaji ya jamii na kuwataka kutenda majukumu yao kwa mujibu wa sheria na maadili ya kitaalamu ili kuleta weledi katika tasnia hiyo.

No comments: