MWANDISHI wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Salma Said, (pichani), ambaye kwa siku mbili alipotea na kuzua sintofahamu, amepatikana.
Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Azam TV kwenye taarifa yake ya habari ya saa mbili usiku huu wa Machi 20, 2016, kikimnukuu kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Siro, kimesema Salma ambaye pia ni mwakilishi wa radio DW ya Ujerumani amepatikana jijini Dar es Salaam.
Salma alitoweka wakati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Karume mjini Unguja, akijiandaa kuja jijini Dar es Salaam kwa matibabu Machi 18,2016
No comments:
Post a Comment