Mkurugenzi wa miradi kutoka ndani ya chama
hicho Bi NASUKI KISAMBU akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika
jijini Dar es salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili kwa pamoja juu
ya maswala ya vufi vitokanavyo na uzazi pamoja na changamoto zake
Na Exaud Mtei(Msaka Habari)
Chama cha wanawake wanasheria nchini Tanzania TAWLA kimeendesha
majadiliano maalum jijini Dar es salaam pamoja na wadau mbalimbali kuhusu
maswala ya vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi na changamoto mbalimbali
zinazowakuta wanawake wakati wa uzanzi nchini Tanzania.
|
Mkutano huo ambao umeendeshwa Jijini Dar es salaam
umewahusisha wadau mbalimbali wa maswala ya kijamii wakiwemo madaktari na
wataalam wa maswala ya uzazi,viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani na wengine
wa mitaa,wanasheria mbalimbali pamoja na wanahabari ambapo lengo likiwa ni
kupanua uelewa zaidi juu ya afya ya uazazi na jinsi gani ya kupunguza Tatizo la
vifo vya wanawake wakati wa uzazi nchini Tanzania.
Akizungumza na wadau huo wakati akifungua mkutano huo
mkurugenzi wa miradi kutoka ndani ya chama hicho Bi NASUKI KISAMBU
amesema kuwa chama cha wanawake wanasheria TAWLA kinaendesha mradi maalum kwa
ajili ya maswla ya matatizo ya uzazni nchini Tanzania mradi ambao unafadhiliwa
na shirika la kimataifa la OXFARM kwa lengo la kusaidia kupunguza vifo
nitokanavyo na uzanzi nchini Tanzania.
Amesema kuwa vifo vingi vyauzanzi wa wanawake nchini Tanzania
vinatokana na na utoaji mimba usio salama ambao unapelekea kupoteza watanzania
wengi kutokana na Tatizo hilo,huku wakiwataka wadau mbalimbali kuliona tatizo
hilo kuwa na kubwa sana na waweze kupambana nalo kwani Linawagharimu watanzania
walio wengi.
Ameongeza kuwa pia lengo na mkutano huo ni
kujadili kwa pamoja haki za wanawake duniani huku wakiangalia pia sheria
mbalimbali zinazowapa haki wanawake hasa katika swala la utoaji mimba na uzazi
kama sheria ya nyongeza ya haki za wanawake ya MAPUTO PROTOCAL na sheria ya
tanzania zinavyozungumza juu ya maswala hayo na utekelezaji wa hizo sheria.
No comments:
Post a Comment