Na Exaud Mtei
Jeshi la polisi kanda
maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 287 ambao ni dada
poa pamoja na kaka poa katika operation maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya
Jiji hilo.
Operation hiyo
ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3 na kuazimia
kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao ambao watakutwa
wakiwanunua.
Katika mkoa wa kipolisi
wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 51 kutoka
katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia
imewakamata jumla ya makaka poa 12 ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka
msimbazi.
Mkoa wa kipolisi wa
temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 22,ambapo changombe
walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa 10.
Aidha katika mkoa wa
kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa kuwakamata madada poa 76
kutoka maeneo ya osyterbay madada poa 49,magomeni 23,na kawe madada poa
4,pamoja na makaka poa 4.
Akizungumza na
wanahabari leo makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamishna wa
kanda hiyo CP SIMON SIRRO amewataka watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja
kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania ambapo amewataka kutafuta biashara
nyingie halali za kufanya.
No comments:
Post a Comment