Wednesday, March 23, 2016

Tigo yatoa msaada wa madawati 500 kwa shule za msingi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada
wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za
msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda(kulia) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (wa pili kulia),wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 500 yalikabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha  ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles (wa tatu kulia)na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dkt. Aziz Msuya(kushoto). Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
 Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada  makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika leo shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Wanafunzi wa shule ya msingi kawawa wakishuhudia makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 
Machi 22 2016 Dar es Salaam: Kampuni ya Tigo
Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5
kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa
kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati
katika shule za msingi nchini.
 
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika
katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo katika kata ya Mabibo katika manispaa ya
Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema mchango huo ni
sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada
mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa
jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari,
wahandisi na wengineo, “amesema Gutierrez.
Gutierrez amesema mwaka jana Tigo
ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya
Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea
kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.
 
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alisema madawati hayo 500 yataboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wito
kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu
katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa
madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Dar es Salaam. Ni dhahiri
kwamba msaada huu wa madawati 500 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata
sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,”
alisema Makonda.

No comments: