Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na
wazee wa mkoa wa Dare s Salaam walipokutana katika kikao ofisini kwake
Leo (Katikati) ni Mwenyekiti wa baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam
Hemed Mkali na kulia ni katibu wa wazee hao Mohamed Mtulia.
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa
Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa
Dar es Salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).
Katibu wa wazee wa Dar es
Salaam Mohamed Mtulia (Kulia) akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu
(kushoto) na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dar es
Salaam Hemed Mkali.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu
cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria
na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii
Rabikira Mushi akizungumza katika kikao kilichojumuisha baadhi ya wazee
wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kulia
ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Sihaba Nkinga.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Dar es
Salaam Bi. Mary Chipungahelo(maarufu kama mama Chips) akichangia mada
katika kikao kati ya baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi na wazee wa mkoa wa Dar es salaam kushoto
ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Sihaba Nkinga na kulia ni Kaimu kamishna Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
…………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imejipanga kuipa nguvu
Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika
changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.
Waziri Ummy amesema wazee
wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema
kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata
mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi
na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.
“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu
hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na
kuipeleka katika Bungeni mwezi Septemba ili tuwe na Sheria
itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusio
wazee” Alisema Mhe.Ummy.
Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa
wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara
ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na
Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania
waishi katika maisha mazuri.
Aidha Waziri Ummy Mwalimu
ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao
kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa
huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na
kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao
unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.
Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa
Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na
Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt
John Pombe Magufuli kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.
No comments:
Post a Comment