Tuesday, March 15, 2016

Tuiweke zanzibar katika maombi--Tizama kilichotokea leo


[​IMG]Pemba hali ni tete, vurugu kati ya maafisa wa polisi na raia zimeripotiwa hii leo huku kukiwa natete kwamba mamia ya wapemba wakikimbilia Mombasa katika nchi jirani ya Kenya.

Ikumbukwe vurugu hizi zinakuja ikiwa ni Siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi visiwani humo ndugu Jecha kutoa waraka wake kwa vyombo vya habari kuwa hali ya usalama visiwani humo ni salama na Amani.

[​IMG]Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba ya Hamdani Omar Makame, Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar tayari imelipuliwa kwa mabomu.
Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata watu waliohusika kwenye tukio hilo.
[​IMG]“Kuna watu wamekamatwa kwa kuhisiwa kuhusika na tukio hilo, bado hali sio shwari mpaka sasa,” anaeleza mwandishi wa habari hizi visiwani humo.
Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo tayari Chama cha Wananchi (CUF), viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati tayari wametoa tahadhari ya kutokea kwa matukio hayo.
Mungu iepushe Tanzania na haya majanga
[​IMG]

No comments: