Wakazi wa kijiji cha Nangoo jimbo la Ndanda wilaya ya Masasi
wamelazimika kusimamisha msafara wa naibu waziri wa maji, Eng Isack
Kamwele kutikana na kukosekana na maji kijijini hapo kwa muda mrefu
ingawa ingawa mradi wa Mbwinji unaanzia kijijini hapo na kuelekea
wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi.
Wananchi hao walibeba mabango yaliyoelezea kukosekana kwa maji na
mengine kuuziwa bei ya Sh500 katika vioski ambavyo vingi vimefungwa
hivyo wananchi wengine kutumia maji ya visima yasiyo salama.
Akitoa malalamiko kwa niaba ya wanakijiji Bakari Amani alisema kuwa
gharama za maji zimekuwa kubwa kuanzia kuunganishiwa pamoja na matumizi
ya kila siku.
"Lugha ya wakala wa Mwanawasa inatukera eti anasema tunapata maji kwa
huruma..pia bei ya maji kwa unit moja ni kubwa mno wapo wanaolipa Sh
1,000 na Sh 2,000 kwa unit,"alisema Amani
Hata Hivyo Naibu Waziri Eng Kamwelwe ameahidi kurudi kijijini hapo
na kutoa ufafanuzi baada ya siku moja kutokana na kuwa nyuma ya ratiba
iliyowekwa.
"Hiki mlichonipa Mheshimiwa mbunge tayari amenieleza na mimi
nitaifanyia kazi lakini kabla lazma nije kuongea na nyinyi Kwa sababu ya
Ratiba nakimbia Nanyumbu Kesho asubuh naamkia Masasi,"alisema Eng
Kamwelwe
Hata hivyo mbunge wa Jimbo hilo Cecil Mwambe aliwaomba wanakijiji hao
kuruhusu msafara huo kuondoka kutokana na ahadi ya Naibu wazir huyo
ambayo ilionekana kuleta matumaini ya upatikanaji wa maji kijijini hapo.
"Tunaomba mruhusu msafara tunakuja kufanya mkutano na nyinyi kesho kujadili maswala ya maji,"alisema Mwambe
No comments:
Post a Comment