Na Exaud Mtei (Msaka
Habari)
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora MH
ANGELA KAIRUKI amesema kuwa lengo la kufikia 50 kwa 50 baina ya wanawake na
wanaume litafikiwa ncini Tanzania endapo watanzania wataipitisha katiba
pendekezwa iwe katiba mpya ya Tanzania kwani imejaa haki za usawa na kijinsia.
Waziri Kairuki ameyasema
hayo leo jijini Dar es salaam katika majadiliano yaliyoandaliwa na mtandao wa
kijisia nchini TGNP kwa lengo la kujadili mambo mbalmbali yanayohusu usawa wa
kijinsia ikiwa ni siku moja kabla ya dunia kuadhimisha siku ya wanawake
duniani,majadiliano ambayo yaliwahusisha wadau mbalimbali wa maswala hayo
Ruth Meena Ni moja kati ya wanaharakati waliotoa mchango wao leo |
Amesema kuwa kwa mujibu
wa katiba pendekezwa imeweka wazi maswala ya usawa wa kijinsia hususani katika
ngazi za uongozi ambapo katika swala la wabunge katiba hiyo imeeleza wazi kuwa
kila jimbo litakuwa na wabunge wawili mwanawake na mwanaume jambo ambalo
litasaidia kuweka haki na usawa wa kijinsia katika nchi.
Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mama MERRY RUSIMBI akizzungumza wakati wa mdalada huo uliofanyika makao makuu ya TGNP Jijini Dar es salaam |
Ameongeza kuwa katika
serikali ya awamu ya tano imeanza kuonyesha mfano kwa kuwajali wanawake kwa
kuanza na kumpa mwanamke nafasi ya kuwa makamu wa Rais jambo ambalo limeanza
kuoonyesha njia na kutia moyo kuelekea malengo ya 50 kwa 50 nchini.
Amesema kuwa lengo la
serikali ni kuhakikisha kuwa wanamuwezesha mwanamke katika secta mbalimbali
ikiwemo swala la kiuchumi na kujikwamua na umaskini,kuwawezesha katika elimu na
kujitambu pamoja na kuwasaidia kuwaondoa katika maswala ya ukatili wa kijinsia.
GENERAL ULIMWENGU ambayo ni mpigania ukombozi nchini alikuwepo |
Katika majadiliano hayo
pia yalihudhruwa na wanaharakati mbalimbali wa maswala ya jinsia akiwemo
GENERAL ULIMWENGU ambayo ni mpigania ukombozi nchini ambapo akizungumza katika
mjadala huo amesema kuwa mila na tamaduni za Tanzania pamoja na kufanyishwa
kazi sana wanawake kuliko wanaume imekuwa ni moja kati ya mambo yanayodidimiza
na na kushusha jitihada za kumwezesha mwananke nchini Tanzania.
Siku ya wanawake Dunia
inaadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8 mwezi kila mwaka wa tatu kote duniani huku kauli mbiu ya
maadhimisho hayo nchini Tanzania 50/50 ifikapo 2030 tuongeze jitihada.
No comments:
Post a Comment