Mtwara.
Wilaya ya Newala na Tandahimba mkoani Mtwara zimetenga fedha za mapato ya
ndani ili kukabiliana na uhaba wa madawati pamoja na madarasa.
Hayo yameelezwa na kiongozi wa kamati ya ufuatiliaji wa miradi
ya maendeleo mkoa wa Mtwara,Amani Rusake wakati wa ziara ya ukaguzi na
kubainisha wilaya ya Tandahimba zaidi ya 150 mil zimetengwa kutoka mapato ya
ndani na mfuko wa elimu kwaajili ya elimu ili kutengeneza madawati mapya na
kukarabati yaliyoharibika.
Alisema kwa wilaya ya Newala kiasi cha Sh 90 mil zimeombewa
kubadilishwa matumizi kwaajili ya utengenezaji wa madawati na wilaya ya
Tandahimba ofisi ya mkurugenzi tayari imeunda kamati kwaajili ya kufuatilia
miti inayofaa kwaajili ya mbao ili kuomba kibali maliasili.
“Mwitikio mkubwa wa elimu bure umepelekea ongezeko la mahitaji
ya madawati na vyumba vya masomo tofauti na ilivyokuwa zamani lakini halmashauri zetu tayari zina
mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto iliyopo kabla ya mwezi June
ikiwa ni utengaji wa pesa
za mapato ya ndani ,"alisema Rusake
Akizungumza mkuu wa shule ya Mdimba kata ya Mnyoma wilaya ya
Tandahimba, Abdallah Majosa alisema kuwa baada ya kutangazwa elimu bure
kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi kuripoti shuleni kama walivyopangiwa.
“Shule yangu inakabiliwa na uhaba wa madarasa na madawati,kidato
cha kwanza wote wanakaa chini,hii imesababishwa na mwitikio mkubwa wa elimu
bure kwasababu wote waliopangiwa wameripoti tofauti na ilivyokuwa miaka ya
nyama kwahiyo kumekuwa na ongezeko la madawati na vyumba vya kusomea,”alisema
Majosa
Akizungumza mtendaji wa kata ya Mnyoma Said Mtondo alisema kuwa
halmashauri tayari imewakata wakulima wa korosho Sh 20 kwa kila kilo wanayouza
kwaajili ya mfuko wa elimu.
“Wakulima tayari walishakatwa na halmashauri Sh20 kila kilo
kwaajili ya mfuko wa elimu kwahiyo sasa hivi kumwambia tena mzazi achangie ni
kitu ambacho kinabidi kiwe
hiari lakini halmashauri tayari kuna mikakati ya kukabiliana na hili ikiwa ni
pamoja na kupasua mbao ili madawati yapatikane,”alisema Mtondo
No comments:
Post a Comment